SERIKALI imedhamilia kuunda mpango mkakati utakaoziwezesha benki nyingi nchini ziweze kutambua hati miliki za kimila ili kuwawezesha wananchi kujikwamua kiuchumi wakitumia hati zao kama dhamana ya mikopo. Azma hiyo imekuja baada ya kuona mafanikio ya kupima na kurasimisha Ardhi katika Wilaya tatu za mfano za Kilombero,Ulanga na Malinyi mkoani Morogoro kulikofanywa na wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya makazi kupitia Programu ya Kuwezesha Umilikishaji Ardhi (LTSP).
Akizumgumza baada ya kutembelea Wilaya za Kilombero na Ulanga akiambatana na wafadhili Wa mradi Wa LTSP ili kuona hatua za utekelezaji Wa mradi,Naibu Katibu Mkuu Wa wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya makazi Mathias Kabundugulu amesema Mradi huo umetekeleza kwa vitendo Sera ya wizara ya miaka mitano.
Amesema kwa kipindi cha miaka miwili toka kuanzishwa kwa mradi Wa LTSP mwaka 2016 mafanikio makubwa yameonekana kwa zoezi kwenda kwa haraka zaidi na wananchi wengi kupata hatimiliki za kimila na za vijiji na hiyo ni kutokana na kwenda na teknolojia mpya ya upimaji ya kutumia simu tofauti na teknolojia waliyoanza nayo ikiwemo ya kutumia GPS.
Amesema kwa kipindi cha miaka miwili toka kuanzishwa kwa mradi Wa LTSP mwaka 2016 mafanikio makubwa yameonekana kwa zoezi kwenda kwa haraka zaidi na wananchi wengi kupata hatimiliki za kimila na za vijiji na hiyo ni kutokana na kwenda na teknolojia mpya ya upimaji ya kutumia simu tofauti na teknolojia waliyoanza nayo ikiwemo ya kutumia GPS.
Naibu Katibu Mkuu huyo amesema kuwa pia amebaini wananchi katika Wilaya hizo wameupokea vizuri mradi na wameonyesha matumaini na imewapanua kiakili hasa baada ya kuelewa kuwa hati hizo wanaweza kuchukulia mkopo baada ya baadhi ya benki kuanza kuzipokea na kuwapatia mikopo.
Mratibu wa Mradi wa kuwezesha umilikishaji ardhi (LTSP) akitoa taarifa fupi ya mradi kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi pamoja na wafadhili wa mradi mjini Ifakara kabla ya kuanza ziara ya uwandani.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mathias Kabundugulu (kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Ulanga Ngolo Malenya (kulia) wakitia saini katika kitabu cha wageni kwenye ofisi ya kijiji cha mbuyuni ambapo pamoja na viongozi hawa, wafadhili wa mradi na wafanyakazi wa LTSP walishiriki katika ziara hii.
Afisa Ardhi mteule wa Wilaya ya Kilombero Syabumi Mwaipopo (alioyeshika karatasi) akiwaelezea Naibu katibu mkuu pamoja na wafadhili mchakato mzima wa kuipata hati ya hakimiliki ya kimila inavyopatikana.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...