BENKI
ya Biashara ya DCB imefanya juhudi za makusudi kuhakikisha inatoka
kwenye hasara iliyopata mwaka 2017 ya Sh.bilioni 1.6 na kurudi kwenye
faida na kwamba baadhi ya hatua zilizochukuliwa ni kuboresha mfumo wa
endeshaji biashara ambapo gharama za uendeshaji zimeshuka na huduma mpya
za kidigitali zimeanzishwa ambapo zimevutia wateja wengi zaidi kufungua
account na hivyo kupunguza kwa kiasi kikubwa gharama zitokanazo na
amana za wateja.
Hayo yameelezwa na Benki ya DCB jijini Dar es Salaam wakati ikitangaza kufanikiwa kupata faida ya Sh. bilioni 1.4 katika kipindi kinachoishia Septemba mwaka 2018 huku ikiipiku hasara ya Sh.bilioni 1.6 iliyopatikana kipindi kama hicho mwaka 2017 ambayo inawakilisha ongezeko la asilimia 187.Faida hiyo ni kwa kipindi cha robo tatu ya mwaka 2018.
Taarifa ya DCB inaeleza kuwa moja ya huduma za kidigitali ambazo benki imezindua ni akaunti ya kidijiti (DCB Digital Account), DCB Kibubu Digital Account na DCB FDR Digital account.Hivyo akaunti hizo zinamuwezesha mteja wao kufungua akaunti na kufanya miamala yote ya kibenki, kutunza fedha na kuwekeza kwa kutumia simu yake ya mkononi.
Kuhusu kukua kwa faida ,benki hiyo imesema kukua huko kwa faida umechagizwa na ukuaji wa mikopo ghafi ya wateja kutoka Sh. bilioni 89.3 Septemba mwaka 2017 kufikia Sh. bilioni 91.3 mwezi Septemba, 2018. Ukuaji huo umechagizwa na utoaji wa mikopo ambapo mikopo ya jumla ya Sh.bilioni 50 imetolewa hadi kufikia Septemba mwaka 2018.
"Idadi ya wateja imeongezeka kutoka 144,445 Desemba mwaka 2017, kufikia wateja 157,366 Septemba mwaka 2018. Mapato halisi ya benki yatokanayo na riba yameimarika katika robo ya tatu ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka uliopita hali ambayo imechagizwa na mkazo wa benki katika kuongeza amana za gharama nafuu kupitia bidhaa za amana za kidijiti, usimamizi wa mizania wenye ufanisi na usimamizi wa gharama za uendeshaji wa benki. Uwiano wa mikopo ghafi na jumla ya amana za benki umeongezeka kwa asilimia 3.1 ikilinganishwa na robo ya pili ya mwaka huu.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...