Na Khadija  Seif, Globu ya jamii                                        
KAMPUNI ya kubashiri michezo ya Sportpesa  imemtambulisha bondia Hassan Mwakinyo ambaye anaongoza katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kuwa balozi wa kampuni.

Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk.Harrison Mwakyembe ameipongeza kampuni ya sportpesa kwa udhamini huo na utakaomuwezesha Mwakinyo kunufaika zaidi.

Dk. Mwakyembe akizungumza zaidi leo Oktoba 26 amesema kuwa mkataba huo hujawahi kutokea tangu sheria mpya ya michezo ya ngumi kutungwa upya na kuwa kama mchezo wa kulipwa.

Amesema kuwa anajivunia kampuni ambazo zinajitolea kwa hali na mali kunyanyua vipaji vya vijana wengi nchini na hata akiondoka madarakani mwaka 2020 atakua ameacha misingi imara itakayowawezesha vijana kujikwamua kiuchumi hasa kupitia sekta ya michezo kwani wengi huendesha maisha yao kupitia michezo ,sanaa na utamaduni.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Utawala na udhibiti wa kampuni ya Sportpesa Abbas Tarimba amesema kampuni hiyo imekua ikitoa udhamini kwa sekta ya mpira wa miguu, hivyo kwa sasa wameona ni vyema kutoa udhamini kwa upande wa michezo ya masumbwi au ngumi.

Tarimba amefafanua zaidi mkataba huo ambao Mwakinyo atapewa ni pamoja na kumgharamikia kuanzia vifaa vyake vya mazoezi pamoja na mahitaji mengine binafsi ili kumpa hamasa kuitangaza sportpesa nchi nzima hata kwa nchi zingine kiujumla. 

Wakati huo huo Makamu Mwenyekiti wa ngumi Alex Mkenyenge ameomba wadau wengi wajitokeze ili kusaidia mchezo wa ngumi kwani kuna vijana wengi wanaofanya vizuri na kupeperusha bendera yetu akiwemo mwakinyo.


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe  akizungumza na waandishi wa habari  katika hafla fupi ya kusaini mkataba wa udhamini na miaka mitatu kutoka  Sportpesa. Kushoto ni Mkurugenzi wa utawala na udhibiti Abas Tarimba na kulia ni Bondia wa masumbwi nchini Hassan Mwakinyo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...