Wakazi wa Jiji la Arusha wameingiwa na hofu kubwa baada ya choo cha shule ya msingi Seliani kutitia na kujeruhi mwanafunzi mmoja huku wengine wakihofiwa kufukiwa. Mkuu wa wilaya ya Arumeru iliyopo mkoani humo, Jerry Murro amewaomba wananchi kuwa watulivu, wakati wa ufukuaji wa vifusi vilivyoporomoka katika choo hicho ili waweze kuona kama kuna wanafunzi wengine wamefukiwa ama la, ingawa inadaiwa kuwa walikuwa zaidi ya mmoja ndani ya choo hicho. Pichani ni jitihada za uokoaji zikiendelea.
Mkuu wa wilaya ya Arumeru iliyopo mkoani humo, Jerry Murro akizungumza na wananchi wa eneo hilo walofika eneo la tukio.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...