Na Khadija Seif, Globu ya Jamii
MWANAMZIKI mkongwe nchini Judith Wambura maarufu kama komando binti machozi lady jdee amewatambulisha rasmi wasanii kutoka nje ambao watatumbuiza usiku wa sauti siku ya leo katika ukumbi wa Mlimani city jijini Dar es salaam.
Aidha , jidee ameeleza ujio wa wasanii wenzake Zahara kutoka Afrika kusini pamoja na Juliana kanyamoze kutoka Uganda kuwa ni kuonyesha hadhira kuwa vipaji bado vinaishi na kukonga mashabiki pia kwani wasanii wakike ni wachache sana na ameona kuwapa fursa hiyo wasanii wakike wapate hamasa na kuendeleza vipaji vyao na kutimiza.
Alikadhalika jidee amekaribisha wasanii wengine kujumuika Kwenye usiku huo na mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Naibu Waziri mwenye dhamana ya habari,sanaa ,utamaduni na michezo Juliana shonza.
Aidha amewataja wasanii kama Damian soul pamoja na grace matata watakuepo Kwenye usiku huo kama wasanii wa ndani ya nchi na ambao wanavipaji lukuki.
Msanii wa kike kutoka nchini Uganda Juliana Kanyamoze amefafanua juu ya kuwa na mashabiki wengi kutoka nchini Tanzania huku akiwa na nyimbo ambazo zinawakonga kutokana na kutumia lugha ya kiswahili wakati hawezi kuongea kiswahili fasaha.
Kanyamoze amesema usiku huo atasherehesha na nyimbo zote alizoimba kwa lugha Kiswahili kwani Zina wapenzi wengi hasa wimbo alioimba na msanii Bushoke wa nchini unaojulikana kama usiende mbali.
Na pia amewaomba mashabiki wakae mkao wa kula kwani kazi yake mpya ataitambulisha hivi karibuni ambayo ni miondoko ya injili.
Mwanamziki
mkongwe nchini Judith Wambura akizungumza na wanahabari wakati wa
kutambulisha wasanii ambao watapamba usiku wa masauti Mlimani city
katika akiwa zuhura kutoka nchi ya afrika kusini ,wa mwisho kushoto ni
msanii Juliana kanyamoze kutoka uganda.

Msanii wa kike kutoka nchini Uganda Juliana Kanyamoze akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...