BENKI ya NMB imesema maboresho
makubwa iliyoyafanya ni matokeo ya mirejesho kutoka kwa wateja wake.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Kitengo cha
Wateja Binafsi wa NMB, Bw. Omari Mtiga alipokuwa akizungumza na Baadhi
ya wateja wa Benki hiyo Tawi la Ilala ikiwa ni mwendelezo wa maadhimisho
ya Wiki ya Huduma kwa Mteja.
"...Maboresho makubwa tuliyoyafanya ni matokeo ya mirejesho kutoka kwa wateja wetu ambayo tumeyapokea siku za nyuma. Siku zote tunatambua na kushukuru kwa michango na maoni ya wateja wetu, ndio sababu ya kuendelea kuwa nao bega kwa bega," alisema Bw. Mtiga.
Aliongeza kuwa NMB inatambua ushindani mkubwa uliopo na itaendelea kukabiliana nao kwa kadri unavyo kua siku hadi siku. Alisema kwao ushindani wanaupenda na wanachukulia kama fursa ya kufanya vizuri zaidi. "...Ushindani ni fursa nzuri maana inatufanya kubuni bidhaa bora kulingana na mahitaji ya wateja na kufanya vizuri zaidi kwa wateja wetu."
Alisema wiki ya huduma kwa wateja tangu ilipoanza NMB imepata fursa ya kujumuika na wateja wake maeneo mbalimbali na kupata mrejesho kwa masuala mbalimbali juu ya huduma zao na ndio maana inachukulia uzito mkubwa kuzungumza na wateja na kutupa mrejesho ili kuweza kuifanyia kazi.
"...Sisi kwetu tunaiona kama fursa ya pekee kukutana na wateja na kupata maoni yao lengo likiwa ni kuboresha zaidi huduma zetu. Lakini tumekuwa tukifarijika zaidi kwani mbali na mrejesho kuna maeneo ambayo wametutia moyo kwamba tunafanya vizuri hivyo tunawaahidi kuongeza juhudi ili kusonga mbele zaidi."
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi Benki ya NMB, Omari Mtiga akimkabidhi cheti maalum Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Chasco Traders, Sando Chasco ambaye ni mteja aliyetukuka wa Benki ya NMB kwa muda mrefu sasa. Mteja huyo amepata mafanikio katika biashara yake baada ya kukuwa na huduma za kibenki za NMB, alianza kukopa shilingi 300,000 na sasa anapata mkopo wa zaidi ya milioni 100 kuendesha biashara zake.

Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi Benki ya NMB, Omari Mtiga pamoja na baadhi ya wateja Benki ya NMB waliojumuika kwenye hafla ndogo ya kuwasikiliza wateja katika tawi hilo wakikata keki maalum ikiwa ni mwendelezo wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja.

Meneja wa NMB Tawi la Ilala jijini Dar es Salaam, Kidawa Masoud akiandaa keki maalum ya wateja kabla ya kuanza kuwalisha wateja wa NMB Tawi la Ilala walioshiriki katika hafla hiyo.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...