Na Stella Kalinga, Simiyu

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Maonesho ya Kwanza ya Viwanda vidogo (SIDO) ambayo Kitaifa yatafanyika mkoani SIMYU katika Viwanja vya nane nane Nyakabindi, kuanzia tarehe 23-28 Oktoba, 2018.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka katika kikao cha maandalizi ya maonesho hayo kilichowashirikisha baadhi ya viongozi wa mkoa wa Simiyu na mameneja wa Shirika la Viwanda vidogo (SIDO) kutoka mikoa ya Simiyu, Dodoma ,Mwanza, Kagera ,Mara, Shinyanga na Arusha.

Mtaka amewakaribisha wananchi wa mkoa mwenyeji Simiyu Watanzania wote kwa ujumla kuja kushiriki maonesho ya SIDO yatakayobebwa na Kauli Mbiu “Pamoja Tujenge Viwanda Kufikia Uchumi wa Kati” na kubainisha kuwa mkoa wa Simiyu unaamini kuwa maonesho hayo yatakuwa ni maonesho darasa, mahali ambapo watu watajifunza na kufanya biashara.

Ameongeza kuwa maonesho ya SIDO yanabeba ajenda ya Serikali ya awamu ya tano na matamanio ya Mhe. Rais ya kuwa na Tanzania ya Viwanda na kuifikisha nchi katika Uchumi wa Kati, hivyo akaawaalika wadau wote wenye teknolojia mbalimbali kushiriki maonesho haya.

“Ninawaalika wadau wote wenye teknolojia mbalimbali waweze kushiriki maonesho haya , nayaalika makampuni, taasisi na mashirika yenye vitu vinavyoweza kuwafaa wajasiriamali na Watanzania ambao wangehitaji kuwekeza kwenye viwanda, waweze kuleta teknolojia zao” .

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na waandishi wa habari na Wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO) Kitaifa,yatakayofanyika mkoani SIMYU katika Viwanja vya nane nane Nyakabindi, kuanzia tarehe 23-28 Oktoba, 2018. 
Baadhi ya na Wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO) Kitaifa,yatakayofanyika mkoani SIMYU katika Viwanja vya nane nane Nyakabindi, kuanzia tarehe 23-28 Oktoba, 2018 , wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ,katika mkutano uliofanyika Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na waandishi wa habari na Wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO) Kitaifa,yatakayofanyika mkoani SIMYU katika Viwanja vya nane nane Nyakabindi, kuanzia tarehe 23-28 Oktob, 2018 . 
Baadhi ya waandishi wa habari na Wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO) Kitaifa,yatakayofanyika mkoani SIMYU katika Viwanja vya nane nane Nyakabindi, kuanzia tarehe 23-28 Oktoba, 2018 , wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ,katika mkutano uliofanyika Mjini Bariadi. 


KUSOMA ZAIDI  BOFYA HAPA>>>>

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...