Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali, Jacob Kingu
(kushoto), akizungumza na Wakuu wa Idara na Taasisi pamoja na maafisa mbalimbali
wa Wizara hiyo, katika kikao cha kupitia taarifa ya utekelezaji wa muundo mpya wa
Wizara hiyo kilichofanyika jijini Dodoma leo. Kushoto kwa Katibu Mkuu, ni Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Ramadhan Kailima, akifuatiliwa na Kamishna Jenerali
wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye. Kulia ni Mkurugenzi wa
Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara hiyo, Issa Ng’imba.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhan Kailima
akizungumza katika kikao cha kupitia taarifa ya utekelezaji wa muundo mpya wa
Wizara hiyo kilichofanyika jijini Dodoma leo. Kikao hicho kilihudhuriwa na Wakuu
wa Idara na Taasisi zilizopo ndani ya Wizara hiyo. Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara
hiyo, Meja Jenerali, Jacob Kingu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali, Jacob Kingu
(katikati), akizungumza na Wakuu wa Idara na Taasisi pamoja na maafisa mbalimbali
wa Wizara hiyo, katika kikao cha kupitia taarifa ya utekelezaji wa muundo mpya wa
Wizara hiyo kilichofanyika jijini Dodoma leo. Watatu kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo, Ramadhan Kailima, na watatu kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na
Rasilimali Watu wa Wizara hiyo, Issa Ng’imba.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali, Jacob Kingu
(wapili kulia), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Ramadhan Kailima (kulia), pamoja
na Wakuu wa Idara na Taasisi pamoja na maafisa mbalimbali wa Wizara hiyo,
wakimsikiliza Mwasilishaji wa taarifa kwa niaba ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, ASF
Athuman Nassa, alipokua anawasilisha katika kikao cha kupitia taarifa ya utekelezaji
wa muundo mpya wa Wizara hiyo kilichofanyika jijini Dodoma leo. Picha na Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...