Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya
maendeleo ya ujenzi wa kiwanda cha kutengenezea Gypsum Board kutoka kwa
Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha Knauf kilichopo Mwanambaya Mkuranga
Bw. Zachopolous Georgions. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua ujenzi wa
barabara Mkuranga – Kisiju inayojengwa kwa kiwango cha lami ikiwa siku
ya tatu ya ziara yake ya siku sita ya kukagua na kuhimiza shughuli za
kimaendeleo mkoani Pwani. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya mpango
wa kuborsha barabra za Mkuranga kutoka kwa Mbunge wa Jimbo hilo ambaye
pia ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (katikati)
wakati akikagua ujenzi wa barabara Mkuranga – Kisiju inayojengwa kwa
kiwango cha lami ikiwa siku ya tatu ya ziara yake ya siku sita ya
kukagua na kuhimiza shughuli za kimaendeleo mkoani Pwani kulia pichani
ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo. (Picha na Ofisi ya
Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia moja ya
vifungashio vinavyotumika kufungashia vigae vya marumaru (tiles)
alipotembelea kiwanda cha Goodwill Ceramic ltd kilichopo Mkuranga mkoani
Pwani, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo na
kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Bw. Robin Huang. (Picha na
Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia ya vigae
(tiles) moja alipotembelea kiwanda cha Goodwill Ceramic ltd kilichopo
Mkuranga mkoani Pwani, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist
Ndikilo na katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Bw. Robin
Huang. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...