Na Mwandishi Wetu,MAELEZO-Bagamoyo

NAIBU Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza amesema Serikali itaendelea kuwajengea uwezo, umahiri na ubunifu wasanii wa Tanzania kupitia Mradi wa Utambuzi wa Wasanii wa Sanaa za Ufundi (TASIP) ili kukuza soko la tasnia hiyo katika ngazi ya kitaifa na kimataifa.

Akifunga Tamasha la 37 la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo, Wilayani Bagamoyo, Mkoani Pwani jana (Jumamosi Oktoba 27, 2018), Shonza alisema malengo ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuhakikisha kuwa tasnia ya sanaa nchini inapiga hatua kubwa zaidi na kuwafanya wasanii kunufaika na kazi zao.

Aliongeza kwa kuzingatia kuwa Wizara yake inasimamia na kutekeleza sera ya sanaa nchini, Serikali itahakikisha kuwa kuipitia mradi wa TASIP unawafikia na kuwatambua wasanii wote nchini na kuwawezesha kuwa na utambulisho rasmi utawaozesha kupata mitaji na mikopo ya kuendesha shughuli zao.

“Mwaka jana nilizindua mradi huu wa TASIP na mwaka huu tumeanza kushuhudia mafanikio makubwa kupitia program hii, kwa kuwa wapo baadhi ya wasanii waliotambuliwa na kusajiliwa na wameanza kupata mikopo kutoka mabenki hatua inayowezesha kupata kutatua baadhi ya changamoto katika kuendesha shughuli zao” alisema Shonza.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Mjasiriamali wa sanaa za uchongaji, Ras Jeshi Beku alipotembelea banda la Msanii huyo wakati wa kufunga tamasha la 37 la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo jana Jumamosi Oktoba 27, 2018, Wilayani Bagamoyo, Mkoa wa Pwani. 
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza (kulia), akitazama kikoi kilitengenezwa na Msajiriamali Esther Mwita alipotembelea banda la Msanii huyo wakati wa kufunga tamasha la 37 la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo jana Jumamosi Oktoba 27, 2018, Wilayani Bagamoyo, Mkoa wa Pwani. 
Naibu Waziri wa Habari, Utanmaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza akitazama moja shati lilitengtenezwa na Mjasiriamali Monica Matemba alipotembelea banda la Mjasiriamali huyo wakati wa kufunga tamasha la 37 la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo jana Jumamosi Oktoba 27, 2018, Wilayani Bagamoyo, Mkoa wa Pwani. 

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza akitazama chungu kilitengenezwa na mmoja wa Wajasiariamali alipotembelea banda la Mjasiriamali huyo wakati wa kufunga tamasha la 37 la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo jana Jumamosi Oktoba 27, 2018, Wilayani Bagamoyo, Mkoa wa Pwani. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...