Serikali
imepiga marufuku uvuvi haramu na kuteketeza nyavu aina ya makokoro 35 ,
makila 6 na nyavu za zenia 25 zilizokuwa zikitumiwa na wavuvi haramu
katika bwawa la Nyumba ya Mungu lililopo wilaya ya Mwanga mkoani
Kilimanjaro
Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kagongo kata Lang’ata leo,Naibu Waziri wa mifugo na Uvuvi Abdalah Ulega
amesema serikali haitamwonea huruma mtu yeyote atakayekamatwa
akijihusisha na uvuvi haramu kwani serikali imekua ikipoteza kiasi
kikubwa cha mapato kutokana na uvuvi huo.
“Hatuna
utani na mtu asiye na huruma na rasilimali za nchi hii, Tanzania ndio
nchi yenye sehemukubwa yenye maji kuliko sehemu nyingine lakini bado
tunaagiza samaki kutoka nchini china, tumeagiza sato., perege hadi kibua
wa kichina, tusipotokomeza leo bwawa litakuwa historia kwa vizazi
vijavyo” amesema Ulega
Kwa
upande wake mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira alisema uwepo wa
bwawa hilo umekuwa msaada mkubwa kwa wananchi katika eneo hilo na sasa
ni wakati wa wananchi kuwa walinzi kwa kila mmoja ili kutokomeza uvuvi
haramu.“Hebu leo amueni kabisa kwamba biashara ya samaki ndio mfumo wa
maisha yenu, Ninyi mkifanya hivyo sisi hatutahitaji kufunga hili bwawa ,
wakati wote tutahitaji kuongeza kizazi cha samaki na kuleta wataalamu
kupima kiwango cha samaki tulichonacho” alisema Mghwira
Kwa
upande wake Dismas Gondwe mkazi wa kijiji cha kigongo kata ya Lang’ata
amesema uvuvi haramu katika bwawa hilo unatokana na kukosekana kwa
utaratibu maalumu unaowaelekeza wavuvi kuendesha shughuli zao katika
bwawa hilo.
Gondwe ameiomba serikali kuwawezesha wavuvi wa bwawa la Nyumba ya Mungu zana harali ambazo serikali inazitambua.
Naibi
Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akizungumza na wavuvi wa
kijiji cha Kagongo kata ya Lang`ata mkoa wa Kilimanjaro kuhusu serikali
kutokumuonea huruma mtu yoyote ambaye atajihusisha na shughuli za uvuvi
haramu.(Picha na Emmanuel Massaka wa MMG Kilimanjaro)
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akiteta jambo na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira.
Naibi
Waziri Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega (wakwanza
kulia) kwa kushirikiana na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira na
Mkuu wa wilaya ya Mwanga Aarron Mbogho wakiteketeza zana haramu
zilizokua zikitumika katika uvuvi haramu kwenye bwawa la Nyumba ya
Mungu.(Picha na Emmanuel Massaka wa MMG Kilimanjaro)
Sehemu
ya wavuvi wa kijiji cha Kagongo kata ya Lang`ata mkoa wa Kilimanjaro
wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega.
Zana haramu zilizokua zikitumika katika uvuvi haramu zikiteketezwa


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...