Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

 HALMASHAURI ya Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha imepata changamoto ya kutitia na kuanguka kwa jengo la choo cha Shule ya Msingi ya Seliani iliyopo kijiji cha Olevolosi kata ya kimnyaki wilayani humo.

Ambapo katika tukio hilo Mkuu wa Wilaya wa Arumeru Jerry Muro kwa kushirikiana na viongozi wengine na wananchi wameweza kuokoa mwanafunzi mmoja wa kiume aliepata majeraha na bado wanaendelea na jitahada za kuondoa kifusi kilichochanganyikana na matofali.

Taarifa iliyotolewa Oktoba 26  na Muro ni kwamba choo ambacho  kimezama  kilikuwa na  matundu 20 .Hivyo katika kukabiliana na changamoto iliyotokea Muro ameliamua kuambatana na Katibu Katibu tawala wa mkoa na viongozi wa halmashauri ya Arusha wamefika eneo la tukio.Taarifa ya Muro ni kwamba baada ya kufika walianza kazi ya kuratibu jitihada za uokoaji wakishirkiana na vikosi vya uokoji na zimamoto pamoja na wananchi wa Kata ya kimnyaki.

"Jitihada hizo tulifanikiwa  kumuokoa mwananfunzi mmoja akiwa amejeruhiwa usoni na kukimbizwa katika hospital ya Seliani kwa matibabu zaidi ambapo mpaka sasa vikosi vya uokoaji vinaendelea na jitihada za kufukua kifusi na matofali yaliyozama katika choo hicho Cha shule chenye matundu 21 ambacho ndio choo pekee kinachotumiwa na zaidi ya wanafunzi 1,121 wa shule hiyo," amesema Muro kwenye taarifa yake.

Amesema katika eneo la tukio kwanza walilazimika kurejesha hali ya amani na kutuliza taharuki za wananchi ambao baadhi wana watoto wanaosoma katika shule hiyo na kutoa nafasi kwa vikosi vya ukoaji kuendelea na zoezi la kutafuta wanafunzi wengine kutokana na kutokupatikana kwa taarifa za awali zinazoonesha idadi ya wanafunzi ambao huenda walikuwa kwenye choo hicho.

Hata hivyo kutokana na shule hiyo kuwa na choo kimoja chenye matundu 20 ambacho ndicho kilikuwa pekee kwa shule hiyo ilimlazimu Mkuu wa Wilaya ya Arumeru kuchukua hatua za kuzungumza na uongozi wa Kanisa la KKKT  Usharika wa Seliani na kuomba shule kutumia vyoo vya Kanisani ombi ambalo lilikubaliwa na Mkuu wa Jimbo la Arusha Magharibi Mchungaji Philemon Joseph Mollel aliyeungana na Mkuu wa Wilaya katika shughuli za uokoaji na hivyo kuondoa Mashaka ya kufungwa kwa shule.

Pia kutokana na kadhia hiyo ilimlazimu Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Muro kuzungumza na wananchi waliojitokeza ambapo katika mazungumzo yake aliwataka wananchi kutulia na kutoa fursa ya kuendelea kwa zoezi la utoaji wa kifusi ili kujirisha na madhara zaidi ambayo huenda yametokea.

Awali baadhi ya wananchi waliungana na Muro katika kuchanga fedha kwa ajili ya kuanza mikakati ya ujenzi wa choo kingine ili kutokwamisha masomo ya wanafunzi kazi ambayo ilifanywa na Mkuu wa Wilaya pamoja na viongozi wa Kanisani na halmashauri na kuitikiwa kwa wingi na wananci wailiotoa Fedha zao.Wakati huo huo Muro alilazimika kumtembelea majeruhi ambae amelazwa katika Hospitali ya Seliani na kumjulia hali huku akiongozana na viongozi mbalimbali.

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe Jerry Muro akimjulia hali mmoja wa wanafunzi aliyejuruhiwa usoni na kukimbizwa katika hospital ya Seliani kwa matibabu zaidi kufuatia kutitia na kuanguka kwa Jengo la choo cha shule ya Msingi ya Seliani katika kijiji cha Olevolosi kata ya kimnyaki Wilaya ya Arumeru 
vikosi vya uokoaji vikiendelea na jitihada za kufukua kifusi pamoja na matofali yaliyozama katika choo hicho Cha shule chenye matundu 20 ambacho ndio choo pekee Kinachotumiwa na zaidi ya wanafunzi 1,121 wa shule hiyo.
vikosi vya uokoaji vikiendelea na jitihada za kufukua kifusi pamoja na matofali yaliyozama katika choo hicho Cha shule chenye matundu 20 ambacho ndio choo pekee Kinachotumiwa na zaidi ya wanafunzi 1,121 wa shule hiyo.
vikosi vya uokoaji vikiendelea na jitihada za kufukua kifusi pamoja na matofali yaliyozama katika choo hicho Cha shule chenye matundu 20 ambacho ndio choo pekee Kinachotumiwa na zaidi ya wanafunzi 1,121 wa shule hiyo. 
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe Jerry Muro akizungumza na wananchi waliojitokeza kushuhutia tukio hilo,ambapo katika mazungumzo yake aliwataka wananchi kutulia na kutoa fursa ya kuendelea kwa zoezi la utoaji wa kifusi ili kujiridhisha na madhara zaidi ambayo huenda yametokea.

KUSOMA ZAIDI  BOFYA HAPA>>>>>>>

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...