Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii. 
WADAU wa Utalii kwa kushirikiana na Vyuo Vikuu katika jiji la Mwanza leo wameanza kampeni ya siku tatu ijulikanayo kama “Discover the Treasures of Mwanza” itakayoshirikisha zaidi ya wanafunzi 800 waliojiunga na vyuo vikuu mwaka huu. 

Lengo la kampeni hii inayotarajia kufanyika katika Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Saanane linatajwa kuwa ni kutoa fursa kwa wanafunzi hao wa elimu ya juu kutambua umuhimu wa kutembelea rasilimali zilizopo nchini na kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa utalii wa ndani. 
 Akizungumzia tukio hili mmoja wa wajumbe wa kamati ya maandalizi ya tukio hilo ambaye pia ni Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustine(SAUT), Judith Wanda,anasema kampeni hiyo inatarajiwa kuanza leo oktoba 26 hadi 28 mwaka huu.
 
 Wanda amefafanua kuwa kupitia kampeni hiyo wanafunzi hao ambao ni wa mwaka wa kwanza watapata fursa ya kubadilishana mawazo na uzoefu kuhusu masuala ya uhifadhi na utalii wa ndani pamoja na namna bora ya kutangaza vivutio vilivyopo nchini. 

 "Vyuo vinaanza udahili hivyo tumelenga wanafunzi wapya wanaojiunga na elimu ya juu na tunatarajia kutumia fursa hiyo kuwafundisha wanafunzi kutembelea vivutio na rasilimali zilizopo nchini kama njia ya kujifunza na tunaamini hawa wataenda kuelimisha jamii umuhimu wa uhifadhi na utalii wa ndani.

 "Kampeni hii ya siku tatu imelenga kukutanisha wanafunzi 800 na kila mwanafunzi atajigharamia kiasi cha Sh 8,800 kwa ajili ya usafiri na shughuli nyingine hifadhini Saanane. Tulishawahi kufanya kampeni ya kwanza na tulikuwa tukihusisha wanafunzi wa maeneo ya Mwanza," 
Kundi la Waandishi wa Habari wakiwa katika boti maalumu kwa ajili ya safari ya kuelekea Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Saanane .
Eneo hili limo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Saanane ambalo linajulikana kama jiwe la kuruka "Jump Stone" limekuwa ni kuvutio kwa wageni walitembelea hifadhi hiyo kwa ajili ya kuchukua Taswira wakati wakiruka.

Baadhi ya Watalii wa ndani wakiwa katika Lango la kuingia ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Kisiw acha Saanane kwa ajili ya kujionea vivutio vya utalii vilivyopo katika Hifadhi hiyo.  




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...