Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii 
WAZIRI wa Fedha na Mipango Dkt.Philip Mpango amesema wadau wamekuwa na mwamko katika sekta ya fedha ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali katika kutekeleza mikakati mbalimbali ya kisera kwa lengo la kuongeza uwelewa na kukuza uwekezaji kupitia masoko ya mitaji. 

Mpango ameyasema hayo wakati wa kutoa zawadi kwa washindi wa shindano kuhusu Masoko na Mitaji kwa wanafunzi wa Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu pamoja na kutunuku vyeti kwa wahitimu wa kozi ya watendaji katika masoko ya Mitaji wanaokidhi viwango vya kimataifa iliyofanyika jijini Dar es Salaam. 

Amesema kuwa masoko na mitaji kuchochea ukuaji wa sekta ya fedha hususani masoko ya mitaji na uchumi kwa ujumla hapa nchini. 

Dkt. Mpango ameiagiza Mamlaka yay a Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) kuendelea kuandaa shindano hilo katika kuwajengea vijana wa kitanzania kujiamini na kuweza kuwa wabobezi katika eneo hilo. 

Amesema shindano hilo kushirikisha wanafunzi zaidi ya 15000 sio kazi ndogo lakini ina manufaa kwa vijana wa kitanzania. 

Nae Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Masoko na Dhamana Nicodemus Mkama amesema kuwa washindi 12 kwa uwiano wa wasichana sita na wavulana sita waliopata alama za juu wamepata fedha sh.milioni 1.8 kwa kila mmoja na kupata safari mafunzo nchini Mauritius kujifunza mamlaka ya usimamizi wa Masoko ya Motaji ya nchi hiyo, Soko la Hisa Mauritius na kampuni tano kubwa za utoaji wa huduma katika masoko ya mitaji. 

Mkama amesema CMSA inaendelea kufanya jitihada za kuongeza idadi wataalam wa masoko na mitaji yenye lengo la kuanzisha na kuendeleza masoko ya mitaji , yenye ufanisi , uwazi na yenye kutoa haki sawa kwa washiriki wote.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango akitoa zawadi kwa washindi wa shindano. 
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Masoko na Dhamana Nicodemus Mkama akitoa maelezo ya shindano hilo lililoratibiwa na Mamlaka hiyo kwa ajili ya kuwapata vijana mahiri wa masoko ya mitaji katika hafla ya utoaji zawadi uliofanyika jijini Dar es es Salaam. 
 Sehemu ya washiriki wa wanafunzi katika shiondano.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...