Na Agness Francis,globu ya jamii 

WAFANYABIASHARA wa Soko la  Samaki Feri jijini Dar es Salaam wametoa ya moyoni kwa kumpongeza na kumshukuru Rais Dk.John Magufuli kwa kutimiza ahadi yake kwa kukabidhi Sh.Milioni 20 kwa ajili ya soko hilo.

Shukrani hizo za wafanyabiashara hao zimetolewa na Diwani wa Kata ya Kivukoni ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya soko hilo Henry Massaba.

Akifafanua zaidi kwa waandishi wa habari kuhusu fedha ambazo zimetolewa na Rais kwa ajili ya wafanyabiashara wa soko hilo ,Massaba amesema  Rais Magufuli ametimiza ahadi aliyoiiahidi kwa wadau hao Desemba 9 mwaka 2015.

"Rais wetu mpendwa alipokuja kufanya usafi katika eneo hili la soko la zone 8 aliahidi  kutoa fedha,na tayari ametimiza ahadi,lazima tumshukuru," amesema.Ameongeza kuwa "fedha hizo Sh. milioni 20 zilizokabidhiwa  kwa wadau wa soko hili zitatumika katika ujenzi wa ofisi ya kikundi cha Umoja wa Wavuvi Tanzania.

Aidha Massaba  amesama  Mama Janeth Magufuli pia aliongezea kutoa mchango mkubwa kwa wakinamama wajasiriliamali wa sokoni hapo ambapo yeye amewakabidhi milioni 5."Fedha hizo zilizotolewa kwa  kinamama hao wa soko hilo la feri zitawasaidia kukuza mitaji na vikundi vyao katika biashara zao,"amesema Massaba .

Kwa upande wa Naibu Katibu wa soko hilo Abeid Bura amewashukuru viongozi wa Serikali ya Awamu ya tano  kwa  kutembelea sokoni na kutambua changamoto na mambo yanayoendelea.
Baadhi ya WAFANYABIASHARA wa Soko la  Samaki Feri jijini Dar es Salaam wakiendelea na shughuli zao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...