Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.


BAADA ya ziara ya siku mbili ya Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya MajiSafi na MajiTaka (DAWASA) Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali Davis Mwamunyange kutembelea mradi wa Chalinze Mbunge wa jimbo hilo aweka wazi msimamo wake na kusema kero ya maji inamalizika.

Akiwa katika ziara ya Mkoa wa Pwani, Halmashauri ya Manispaa ya Chalinze Jenerali Mwamunyange aliweza kutembelea mradi wa Chalinze akiambatana na mbunge wa Jimbo hilo Ridhiwani Kikwete.

Akizungumza baada ya kukagua mradi huo wa ujenzi wa Matenki 19, ulazaji wa mabomba ya ukubwa mbalimbali kwa kilometa 1, 203, ujenzi wa vizimba vya kuchota maji pamoja na upanuzi wa mtambo wa kusafisha maji wa Chalinze ukiwa na Lengo la kuongeza uzalishaji kufikia mita za ujazo 900 kwa siku kutoka mita za ujazo 500, Mbunge Rudhiwani kikwete ameishukuru serikali kwa kuja kuona hali halisi ya upatikanaji wa maji jimboni kwake.


Ridhiwani amesema kuwa hatua ya Mwenyekiti wa Bodi kutembelea chanzo cha maji cha Chaliwasa kwani kilio kimefika na kuanzia sasa yale matatizo ya maji yatakwisha.Amesema kuwa, anaipongeza serikali kwa kuweka utaratibu mpya wa kutenga akaunti maalumu ya kupokea pesa za miradi na hilo litasaidia kukamilika mradi kwa mapema zaidi.

Ridhiwani amesema, yale malengo mazuri ya kupata maji kabla ya 2019 yatafikiwa kama matarajio ya wananchi kupata maji muda wote. Katika ziara hiyo, Jenerali Mwamunyange amewataka kampuni ya Jain Irrigation System kukamilisha mradi huo kufikia Desemba 30 kwani wameshawapa muda mwingi na bado hawajakamilisha.

Kazi hii itakapokamilika, wakazi waliopo maeneo ya Manga hadi Tengwe katika Mkoa wa Tanga; mji na vitongoji  vya wa Chalinze na baadhi ya maeneo ya Bagamoyo na Kibaha katika mkoa wa Pwani watafaidika.

 Mradi pia utanufaisha baadhi ya maeneo ha Mkoa wa Morogoro ikiwa ni pamoja na  maeneo ya Kizuka A na B, Ngerengere, Kinoko A and B, Tukamisasa, Lulenge, Visakazi hadi Bwawani  pamoja na Sangasanga A na B. Hadi utakapokamilika, mradi utagharimu dola za Marakani 41,362,023.43 ambazo ni mkopo wa masharti nafuu kutoka Serikali ya India kupitia Benki ya EXIM ya India.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mradi wa maji wa Chalinze utakaowapatia maji ya kutosha wananchi ya jimboni kwake
 Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali Davis Mwamunyange akipata maelezo mbalimbali kutoka kwa Meneja wa Mradi huo P. G. Rajon wakati wa ziara yake katika mradi wa Chalinze.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...