Na Leandra Gabriel, blogu ya jamii

Elimu kuhusiana na namna ya kujikinga na kansa kwa wenye ulemavu wa ngozi imetakiwa kufika katika maeneo yote nchini ili kuweza kuwakinga na kupata matatizo ya kansa ya ngozi.

Akizungumza na blogu ya jamii Mwenyekiti wa watu wenye ualbino Wilaya ya Ilala Seif Ulate ameeleza kuwa tatizo kubwa linalowaondoa duniani ni kansa na hii ni kutokana na athari za jua akitolea mfano wa kanda ya ziwa ambako shughuli zao ni kilimo na uchungaji ambazo ni za kukaa muda mrefu juani hali inayopelekea kupata kansa kwa urahisi zaidi.

Akieleza hali ya kansa kwa jiji la Dar es salaam Ulate amesema kuwa wanawake jijini hapo huongoza kwa kufa kwa kansa na kwa mwaka huu takribani wanawake 8 wamefariki kwa ugonjwa huo na hiyo ni kutokana na kuiga kwa mitindo ya maisha kutoka kwa wanawake ambao hawana ualbino hasa katika mavazi na nywele bila kujali hali yao ya ngozi.

Aidha amesema kuwa licha ya kuwepo kwa chama hicho ila bado elimu haijafika hasa katika maeneo ya vijijini na ameiomba serikali kuhakikisha elimu kuhusu wao inaenea nchi nzima hasa katika kuwakinga watoto wenye ualbino kwa wazazi, walimu kuwa na uelewa juu ya uoni hafifu walionao na kutoa kipaumbele wawapo darasani na wazazi kutowatenga na kuwabagua watoto kutokana na hali ya ngozi zao.

Pia ameiomba serikali kuongeza idadi ya chupa za mafuta wanayotumia ili kulinda ngozi zao na amesema kuwa  kwa kuwa hiyo ndio dawa inayowasaidia hivyo hayana budi kupatikana muda wote na kila  sehemu nchini hasa vijijini.

Ulate ametoa wito kwa watu wenye ulemavu wa ngozi kuishi katika mitindo bora ya maisha inayoendana na hali za ngozi zao hasa kujikinga na jua.
Badhi ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino) wakiwa kwenye moja ya mikutano yao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...