Katika dhamira yake ya kuhakikisha Watoto wa kike wanapata elimu kuhusu umuhimu wa usafi katika kipindi vya hedhi, taasisi ya Her Africa imezindua kampeni ya kitaifa inayojulikana kama “Hedhi yangu, Furaha yangu” katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike ambayo huadhimishwa tarehe 11, Oktoba kila mwaka kama ilivyopangwa na Umoja wa Mataifa (UN).
Kupitia kampeni hii mifuko maalum itatolewa kwa wasichana ambao ndani yake kukiwa na mahitaji muhimu katika kipindi cha hedhi kama vile, paketi za pedi za kutumia mara moja na za kutumia zaidi ya mara moja, vitambaa laini vya kujisafishia, chupi na khanga mpya, sabuni ya kuogea pamoja na ya kufulia na dawa ya Dettol.
Vifaa vinavyopatikana katika kifurushi hiki vimetolewa na wadau mbalimbali katika jamii kama msaada kutokana na jitihada kubwa zilizofanywa kupitia mitandao ya kijamii na taasisi ya Her Africa kufanya uhamasishaji wa kulielezea tatizo na kutafuta kuungwa mkono kulipatia ufumbuzi.
Vifaa vinavyopatikana katika kifurushi hiki vimetolewa na wadau mbalimbali katika jamii kama msaada kutokana na jitihada kubwa zilizofanywa kupitia mitandao ya kijamii na taasisi ya Her Africa kufanya uhamasishaji wa kulielezea tatizo na kutafuta kuungwa mkono kulipatia ufumbuzi.
Meneja Miradi wa Her Africa, Salha Kibwana amesema “Wanawake wengi na wasichana katika jamii zetu hupata changamoto kubwa katika kipindi cha mzunguko wao wa mwezi wa siku za hedhi, kutokana na kutoweza kumudu kununua pedi za kutumia, ukosefu wa elimu kuhusiana na hali hiyo, imani za mila ambazo zinawafanya wengi kuamini kuwa suala la hedhi halipaswi kuongelewa, ukosefu wa mazingira rafiki ya kujihifadhi mtu anapokuwa kwenye hali hiyo kama vile vyoo na maji safi ya kutumia. Changamoto hizo zote zinasababisha watumie vifaa vya kuwasitiri visivyofaa ambavyo vinaweza kuwasababishia kupata maradhi.”
Naye Zena Tenga, kutoka taasisi hiyo ya Her Africa, aliongeza kusema “Kampeni yetu hii imelenga kutoa elimu ya ufahamu kuhusiana na umuhimu wa usafi katika kipindi cha hedhi, kuwezesha kufahamu mzunguko wa siku za hedhi kwa mwezi kwa ajili ya kujiandaa, kujua dalili za kuingia kwenye siku za hedhi na mengineyo mengi.”
Moja ya mwanzilishi wa mradi wa " Her Africa" akizungumza na wanafunzi wa kike kutoka shule ya primary St Joseph kuhusu elimu hedhi kabla ya kutoka msaada wa mifuko maalum kwa wasichana hao yenye vitu muhimu vya kutumia wakatika wa kipindi cha hedhi.
Wanafunzi kutoka shule ya msingi ya St Joseph wakionesha mifuko maalum waliyopokea kutoka kwa "Her Africa" yenye vitu muhimu vya kutumia wakatika wa kipindi cha hedhi. Her Africa imeanzisha kampeni ya "Hedhi yangu, Furaha Yangu" ambayo inatarajia kuwafikishia wasichana 600 mifuko hiyo maalum yenye vifaa vya hedhi.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...