Uongozi wa Chuo cha Kimataifa cha Sayansi na Biashara cha Nchini Oman umekusudia kuanzisha chuo chengine kipya cha Kimataifa Visiwani Zanzibar kitachopewa jina la American and Europe of East Africa kwa lengo la kutanua Sekta ya Elimu ndani ya Ukanda wa Afrika Mashariki.
Mkuu wa Chuo cha Sayansi na Biashara cha Nchini humo Dr. Muneer Moh’d Al – Naamany alitoa kauli hiyo wakati Ujumbe aliouongoza wa Chuo hicho ulipofanya mazungumzo na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Vuga Mjini Zanzibar.
Dr. Muneer Moh’d Al – Mastar alisema Zanzibar lazima iwe kituo cha Elimu katika Ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Bara la Afrika kitakachomjengea uwezo wa ajira ya kuaminika mahali popote Duniani Mwanafunzi aatakayemaliza masomo yake kwenye Chuo hicho.
Alisema mazingira ya kumfinyanga Mwanafunzi katika muelekeo wa chuo hicho kinachokusudiwa kuanzishwa Zanzibar unatokana na uzoefu wa miaka 20 tokea kuanzishwa kwa Chuo chao chenye Wahadhiri kutoka pembe zote za Dunia wanaofundisha kwenye Taasisi yao.
Mkuu huyo wa Chuo cha Sayansi na Biashara cha Oman mwenye Asili ya Zanzibar alimueleza Balozi Seif kwamba Uongozi wa Chuo chake umefikiria Mpango huo kwa nia ya kuirejeshea hadhi yake Zanzibar kuwa Kituo cha masuala mengi katika enzi zilizopita hasa harakati za Biashara na usafiri uliokuwa ukiunganisha Dunia.
Naye kwa upande wake Naibu Mkuu wa Chuo cha Sayansi na Biashara cha Nchini Oman Dr. Ahmed Al – Naamany alisema mfumo wa ufundishaji utakaotumika utampa uwezo Mwanafunzi kuendelea na masomo yake hata akiwa nje ya Zanzibar.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Kulia akizungumza na
Uongozi wa Chuo cha Kimataifa cha Sayansi na Biashara cha Nchini Oman
uliofika Ofisini kwake Vuga kwa mazungumzo ya kuataka kuanzisha Chuo
Kikuu Visiwani Zanzibar.
Mkuu
wa Chuo cha Sayansi na Biashara cha Nchini humo Dr. Muneer Moh’d Al –
Naamany wa Pili kutoka Kulia akielezea msimamo wa Uongozi wa Chuo chake
kutaka kuanzisha Chuo Kikuu Visiwani Zanzibar.
Dr.
Muneer Moh’d Al – Naamany akisisitiza jambo wakati akizungumza na
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Vuga Mjini
Zanzibar.
Naibu
Mkuu wa Chuo cha Sayansi na Biashara cha Nchini Oman Dr. Ahmed Al –
Naamany akimueleza Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mh.
Riziki Pembe Juma aliyeshiriki mazungumzo hayo fursa zitakazopatikana
katika mafunzo yatakayotolewa na Chuo hicho.
Dkt. Muneer Moh’d Al – Naamany akifafanua zaidi malengo ya Chuo chake
mbele ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Vuga
Mjini Zanzibar.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...