BENKI ya Amana na Kampuni ya TY Services Limited inayoendesha mtandao wa Taxify nchini zimesaini mkataba wa kuwawezesha madereva 50 wa mtandao huo kumiliki magari. Hayo yamesemwa  jijini Dar es Salaam na Meneja Biashara wa Benki ya Amana Dassu Mussa wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kusainiana mkataba huo.

Mussa alisema benki hiyo imejipanga kuwezesha jamii ya Kitanzania kuondoka katika wimbi la umaskini hivyo mkataba huo utafungua njia ya kiuchumi.  Alisema benki hiyo inayoendeshwa kwa kuzingatia mfumo wa kiislam hatua hiyo ya kushirikiana na Taxify ni sehemu ya mikakati ya kuwa benki kiongozi katika kutoa hiding za kibunifu. 

"Uwezeshaji huu utakuwa wa vikundi vya madereva 10 ambao watadhaminiana wenyewe na ataweka dhamana isiyopungua asilimia 10 ya thamani ya chombo anachohitaji kuwezeshwa, na dhamana hiyo itatumika hadi kumaliza marejesho,"alisema.
Alisema mkataba huo unamtaka dereva aweke akiba ya Sh. 15,000 kwa wiki ambayo itakuwa dhamana hadi dereva atakapokamilisha rejesho miaka miaka miwili.

"Benki itazingatia vigezo mbalimbali katika kutoa uwezeshaji huo ikiwemo dereva kuwa na uzoefu wakutosha,"alisema.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkazi wa TY Services, Remmy Eseka alisema ushirikiano huo ni chachu ya kuongeza ajira kwa Watanzania. Eseka alisema mtandao wa Taxify upo katika mikoa mitatu ya Dar es Salaam, Mwanza na Dodoma hiyo ujio wa Amana katika huduma hiyo ni fursa muhimu.

"Tumejipanga kutumia fursa hii ya Amana Benki kuwezesha madereva wa taxify nchini naamini utakuwa mchango mkubwa kwa uchumi wa nchi,"alisema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...