Benki
ya Stanbic Tanzania imezindua mfumo utakaoruhusu mauzo na manunuzi ya
fedha za kigeni kimtandao uitwao ‘eMarket Trader’. Hii ni jitihada ya
benki hiyo kuwapatia wateja wao huduma mahususi katika kubadilisha fedha
za kigeni, huduma hii inajumuisha wateja binafsi pamoja na makampuni
makubwa na madogo. Kupitia mtandao huu, wateja wanaweza kujua taarifa za
thamani ya fedha za kigeni kwa wakati husika pia kupata taarifa juu ya
mwenendo wa soko.
Huduma hii ni ya kwanza na ya kipekee nchini Tanzania na inapatikana mtandaoni. eMarket Trader inawawezesha wateja kubadilisha fedha zao kwa urahisi zaidi na kuwapatia zaidii ya aina 64 za fedha zilizopo sokoni kwa wakati huo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi, Meneja wa Masoko ya fedha kutoka Benki Kuu (BoT), Bw Lameck Kakulu alisema “Tunafuraha kuona benki ya Stanbic, moja ya wadau muhimu katika sekta ya fedha nchini wakijikita katika teknolojia. Kupitia uboreshaji huu wenye vipengele muhimu vya kidijitali kama kupata taarifa za soko katika muda halisi na upatikanaji wa tafiti za Benki ya Standard Bank.”
“Hapo zamani wateja wetu walihitaji kupiga simu kitengo cha ubadilishaji fedha kwa ajili ya kununua au kuuza fedha zao, na huduma hii iliwezekana tu wakati wa saa za kazi za benki. Hivyo basi, kupitia e-Market Trader, wateja wetu wanaweza kubadilisha fedha zao na kupata taarifa juu ya soko kwa wakati” alisema Mkuu wa Kitengo cha Masoko ya Fedha za kigeni wa Benki ya Stanbic, Bw Erick Mushi.
Bidhaa hii imelenga kuhakikisha wateja wote wa Benki ya Stanbic ambao biashara zao zinahusiana na masoko mbali mbali ya kimataifa wanapata maendeleo ya kifedha. Mpaka sasa miamala inayofanyika katika mtandao huu kwenye benki za Stanbic Africa ni dola za Kimarekani bilioni 18 na watumiaji zaidi ya 5,000 huwepo mtandaoni kila siku. Uzinduzi huu unaashiria utekelezaji wa ahadi iliyowekwa na Benki ya Stanbic ambayo ni kuchochea maendeleo ya wateja wake na Tanzania kwa ujumla.

Meneja
wa Masoko ya fedha kutoka Benki Kuu (BoT), Bw Lameck Kakulu akizindua
huduma ya soko la fedha za kigeni kidijitali ya Benki ya Stanbic iitwayo
eMarket Trader jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.
Wengine ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko ya Fedha za kigeni wa Benki ya
Stanbic, Bw Erick Mushi (kulia) na Mkuu wa Huduma za kibenki za
mashirika na uwekezaji wa Benki ya Stanbic Bw Manzi Rwegasira.
Meneja
wa Masoko ya fedha kutoka Benki Kuu (BoT), Bw Lameck Kakulu akipeana
mkono na Mkuu wa Kitengo cha Masoko ya Fedha za kigeni wa Benki ya
Stanbic, Bw Erick Mushi (kulia) baada ya uzinduzi wa huduma ya soko la
fedha za kigeni kidijitali ya Benki ya Stanbic iitwayo eMArket Trader
jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyopita. Katikati ni Mkuu wa
Huduma za kibenki za masharika na uwekezaji wa Benki ya Stanbic Bw Manzi
Rwegasira.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...