Zaidi ya wataalamu 600 katika sekta ya afya nchini Tanzania and kwingineko duniani wanakutana jijini Dar es Salaam kwenye kongamano la 5 la afya (Tanzania Health Summit) linaloanza Novemba 13(kesho). Litahitimishwa Jumatano Novemba 14. Kwa mara ya kwanza, kongamano hili lilifanyika nchini mwaka 2014.
Kongamano la mwaka huu linakuja na fursa mbalimbali kwa wadau wote walioko katika mfumo mzima wa afya nchini. Viongozi wa serikali, wawekezaji, watafiti na wabunifu watakutana kujadili mada kuu kuhusu dira ya Tanzania katika kuelekea uchumi wa viwanda. Kaulu mbiu ya mwaka huu ni, Ukuaji wa viwanda nchini Tanzania: Tathmini ya ukuaji na jinsi ya kutatua changamoto zilizokithiri.
Waandaaji na waratibu wa kongamano hili ni TAMISEMI), Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Wizara ya Afya ya Zanzibar, BAKWATA na Tume ya Kuratibu Huduma zitolewazo na makanisa (CSSC), Tindwa Medical and Health Services na Wasimamizi wa Hospitali za Binafsi(APHFTA).
Wataalamu wa afya kunufaika
Kwa mara ya pili, wataalamu wa afya nchini watakao hudhuria kongamano na watakaowasilisha machapisho yao watapewa alama za kufuzu viwango vya kitaaluma. Hii itawasaidia kukuza taaluma zao na kuongeza alama za ujuzi katika kile kinacho itwa Continuing Professional Development (CPD).
Kongamano la afya la Tanzania (THS) limepewa ithibati ya kutoa alama hizo na Chuo kikuu ya tiba na sayansi shirikishi(Muhas). Hii ni baada ya serikali, kupitia wizara ya afya, kutoa mwongozo kwamba wataalu wa afya ni lazima watafute njia za kujiendeleza kitaaluma wawapo makazini ili kukuza ujuzi na weledi katika taaluma zao.
Rais wa Kongamano la Afya Tanzania, Dkt Omary Chillo, amesema, “Wataalamu wa afya wasibweteke baada ya kupata na kuanza kufanya kazi. Utaalamu huwa unapotea taratibu na baada ya muda. Bila kuongeza ujuzi kitaaluma wataalamu wengi wanaweza kujikuta wakibaki nyuma. Haijalishi kama wana uzoefu kiasi gani. Kuna mabadiliko makubwa katika teknolojia za tiba na utandawazi. Kongamano hili ni fursa pekee kwa hivi sasa kujieongezea alama kitaaluma.”
Zaidi ya taasisi 100 kushiriki, watoa mada 40
Zaidi ya taasisi 100 zinashiriki katika kongamano hili. Katika majukwaa yaliyoandaliwa katika ukumbi wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), taasisi ya JHPIEGO itaonyesha mbinu maalumu ya kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi usio salama hapa nchini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...