Frank Mvungi- MAELEZO 

Serikali kutumia zaidi ya Bilioni 67 katika ujenzi wa Daraja la mto Wami na linatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 24 na hivyo kuchochea ukuaji wa sekta ya uchukuzi hapa nchini. 

Akijibu swali la kuhusu ujenzi wa Daraja hilo, Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Elias Kuandikwa amesema kuwa kwa sasa Mkandarasi yupo kwenye maandalizi ya kuanza ujenzi ambapo baada ya maandalizi hayo kazi ya ujenzi wa daraja utaanza ukigharimiwa na Serikali kwa asilimia 100. 

“ Wakati wa Barabara Tanzania (TANROADS) na Mkandarasi Power Construction Corporation kutoka China walisaini mkataba wa ujenzi wa daraja hili tarehe 28/05/2018 hivyo tayari kazi ya ujenzi inatarajiwa kuanza wakati wowote”; Alisisitiza Mhe. Kuandikwa 

Akifafanua Mhe. Kuandikwa amesema kuwa Daraja jipya la Wami litakuwa na urefu wa mita 513.5 na upana wa mita 11.85 na litajengwa umbali wa mita 670 pembeni ya daraja la zamani upande wa kulia ukiwa unaelekea Segera. 

Aliongeza kuwa upana wa daraja hilo umezingatia sehemu ya barabara, waenda kwa miguu pamoja na vizuizi kwa ajili ya usalama. Daraja hilo litakuwa kichocheo cha maendeleo katika mikoa ya Kaskazini kwa kuchochea shughuli za usafirishaji na uchukuzi kwa njia ya barabara. 

Daraja la sasa la mto Wami lenya urefu wa mita 88.75 liko mkoa wa Pwani na lilijengwa mwaka 1959 na ni kiungo muhimu kutoka Chalinze kwenda mikoa ya ukanda wa Kaskazini mwa nchi yetu na nchi za jirani. 
Daraja la Wami 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...