Na Ahmed Mahmoud Arusha .

Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro amewataka waalimu na Afisa elimu kuhakikisha mpango wa KKK (LANES) unatiliwa mkazo sanjari na kuhakikisha wanafunzi wanajua kusoma kuandika na kuhesabu ili kuleta matokeo chanya na kufikia malengo ya serikali ya wananchi wote kujua kusoma. 

Akiongea wakati akifungua wiki ya kusoma na stadi za kukuza kusoma kuandika na kuhesabu (LANES) iliyofanyika katika Maktaba ya mkoa Dc Daqarro amesema kuwa wajibu huo ni wetu sote kuanzia nyumbani hadi mashuleni kuhakikisha kila moja wetu anatimiza wajibu wake. 

Amesema kuwa wiki kama hiyo ni ya kujitathmini tumefika wapi na tunaelekea wapi kama taifa kwa ajili ya kukuza uelewa wa vijana wetu kujua kuhesabu kusoma na kuandika ili kuwa na taifa linalopiga hatua kwa wananchi wake kujua kusoma. 

“Taifa limejipanga kuondoa wananchi wasio jua kusoma na kuandika ndio maana ilikaja na mkakati wa kkk hivyo kila mmoja wetu anawajibu kuhakikisha tunafikia malengo ya mkakati huu”alisema Daqarro
Kwa Upande wake Afisa elimu vielelezo Godfrey Augustino amesema kuwa wajibu wa wazazi ni kufuatilia maendeleo ya watoto wao na wao kama waalimu watahakikisha kila kijana anayepata nafasi anajua kusoma kuandika na kuhesabu lengo ni kuondoa vijana wanaomaliza elimu wakiwa hawajui kusoma na kuandika. 
Mkuu wa wilaya Arusha mjini Gabriel Daqarro akifungua wiki ya usomaji iliyofanyika kwenye maktaba ya mkoa Arusha pembeni ni mkutubi mkuu wa maktaba hiyo Bi Rafiki Mvamba na kushoto ni Afisa elimu Vielelezo Godfrey Augustino wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi mkuu huyo wa wilaya
Afisa elimu Vielelezo Godfrey Augustino akitoa hotuba kwenye ufunguzi wa wiki ya usomaji Lanes kabla ya kumkaribusha mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro 
Meza kuu wakiwa wanajadiliana mkuu wa wilaya na mkutubi mkuu wa maktaba bi Rafiki Mvamba ambapo afisa elimu akiendelea kutoa hotuba yake kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi 
Pichani juu na chini ni sehemu ya wanafunzi wa shule sita za wilaya ya Arusha walioshiriki mashindano mbali mbali ya kusoma kuandika na kuhesabu wanaoonekana pichani ni wanafunzi wa shule ya msingi Mwangaza na sombetini wakifuatilia kwa makini matukio mbali mbali yalioendelea kwenye hafla hiyo .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...