*Biteko asema wachimbaji sasa kuchimba kwa uhakika

Na Asteria Muhozya, Dodoma

Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) imetakiwa kuandaa ramani zinazoonyesha madini mbalimbali katika ngazi ya Mikoa na Wilaya ili kuwapa nafuu watanzania wanaofanya shughuli za uchimbaji wa madini nchini.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko baada ya kupokea taarifa ya Utafiti wa Jiokemia katika skeli kubwa na skeli ndogo (Geochemical Mapping for High and Low Density) uliofanyika nchi nzima kwa ushirikiano kati ya GST na Taasisi ya Jiolojia ya China.

Naibu Waziri Doto pia, ameitaka taasisi hiyo kuelekeza nguvu katika kuisaidia serikali katika kupata matokeo chanya katika shughuli za madini huku ikiongeza thamani ya kazi kutokana na utafiti huo na kuongeza kuwa, GST inaweza kutumia utafiti huo mkubwa kuandaa ramani za madini katika ngazi za Mikoa na Wilaya.

Akizungumzia manufaa ya tafiti huo kwa Tanzania, amesema baada ya muda si mrefu watanzania wanaofanya shughuli za uchimbaji watahamia katika uchimbaji wa uhakika na siyo wa kubahatisha kwa kuwa utafiti huo unaonesha mahali sahihi ambapo shughuli hizo zinaweza kufanywa.

Amesema mbali na shughuli za madini, utafiti huo pia unaweza kutumika katika sekta za kilimo, maji na ujenzi wa barabara kwa kuwa unawezesha kutambua aina ya udongo unaofaa kwa shughuli hizo. 

Kutokana na umuhimu wa utafiti na kazi iliyofanywa na taasisi hizo mbili, Naibu Waziri Biteko ametoa wito kwa Watanzania kuitumia taasisi ya GST katika shughuli za kitaalam ikiwemo kupata taarifa za utafiti zinazohusu sekta ya madini na kuongeza kuwa, sekta hiyo inao uwezo mkubwa wa kutekeleza wajibu wake.Aidha, Naibu Waziri Doto ametumia fursa hiyo kuishukuru Serikali ya China kutokana na ushirikiano huo iliyoutoa katika kutekeleza utafiti huo ambao umegarimu kiasi cha Dola za Kimarekani Milioni 4 na Laki Tano 
 Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko, akionesha taarifa ya utafiti wa jiokemia uliofanywa nchi mzima na Taasisi ya Jiolojia ya Madini Tanzania (GST) kwa kushirikiana na Taasisi ya Jiolojia ya China. Kulia ni Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Jiolojia ya China Profesa Sun Xiaoming na Kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Mathias Absai.
 Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka Taasisi ya Jilojia ya China, Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST), na Wataalam kutoka Wizara ya Madini na Tume ya Madini.
 Naibu Waziri Doto Biteko akimkabidhi Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Jiolojia ya China, Profesa Sun Xiaoming Cheti cha kutambua mchango wake na kukamilika kwa utafiti wa Jiokemia uliofanywa nchini.

 Sehemu ya Wataalam kutoka Taasisi ya Jiolojia ya China, Wizara, Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) na Tume ya Madini wakifuatilia kikao hicho.

KUSOMOA ZAIDI BOFYA HAPA>>>

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hiki ni kitu kizuri sana.Pongezi sana kwa waliobuni wazo hili.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...