Kamishna wa Bima Nchini, Dkt. Baghayo Saqware amefanya mazungumzo na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Prof. Mussa Juma Assad yaliyolenga kukuza ushirikiano wa usimamzi wa sekta ya bima na ukaguzi wa hesabu za serikali.

Akizungumza na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali mwishoni mwa wiki, Dkt. Saqware alisema Mamlaka ya Usimamizi wa shughuli za Bima (TIRA) imefanya mabadiliko madogo ya sheria ya bima Na. 10 ya Mwaka 2009 katika kifungu cha 133, kinachotaka majanga yote ya yapewe kinga na makampuni ya Bima yaliyosajiliwa na Mamlaka, na kuomba Ofisi ya CAG kuweka utaratibu wa ukaguzi wa utekelezaji wake kwenye miradi ya serikali.

“Ndugu CAG, mabadiliko haya yanataka majanga yanayotokana na
uendashaji wa shughuli zote za kiuchumi na kijamii kukatiwa bima na
makampuni yenye usajili nchini, ndiyo sababu serikali imeona ni vema
tushirikiane katika kuhakikisha taasisi zetu zinakidhi matakwa ya
sheria hii” alisema Dkt. Saqware.

Serikali ya Awamu ya Tano inatekeleza miradi mingi na mikubwa ya
kimkakati hivyo ni fursa adhimu kwa kwa sekta ya bima kushiriki
kikamilifu katika kuhakikisha miradi hii inapatiwa kinga dhidi ya
majanga yanayoweza kuathiri na kuchelewesha utekelezaji wa Miradi
hiyo
.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...