Mawaziri wa sekta za uchumi wamekutana Jijini Dodoma kujadili utekelezaji wa Programu ya pamoja ya Ujenzi wa Uchumi wa Viwanda.

Akizungumza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama ambaye alikuwa Mwenyekiti wa mkutano huo alisema kuwa Programu ya ujenzi wa uchumi wa viwanda imejikita katika kuweka mazingira wezeshi ya biashara na uwekezaji nchini kwa lengo la kuvutia sekta binafsi na kuongeza fursa za ajira.

“Programu hiyo itakuza uchumi na ujenzi wa viwanda kwa kufuata misingi na kanuni za kibiashara zinazokubalika kimataifa, ikiwakama nyenzo muhimu katika kuhakikisha viwanda vitakavyoanzishwa vinakuwa chachu ya maendeleo hapa nchini,” alisemaMhagama.

Aliongeza kuwa Serikali imedhamiria kutekeleza kwa vitendo azma ya ujenzi wa uchumi wa viwanda ili kufikia malengo ya dira ya Taifa ya maendeleo ya kuiwezesha Tanzania kuwa nchi ya kipato cha kati ifikapo 2025.
Hata hivyo, Waziri Mhagama alieleza kuwa Programu hii ya pamoja inatokana na kutegemeana kwa mipango na mikakati ya kisekta katika kufikia malengo ya Serikali kwa pamoja.

Aidha, alitoa rai kwa kila mmoja kuhakikisha sekta anayoiongoza inatoa mchango stahiki katika kufikia azma ya Serikali kwa kuweka malengo yanayotekelezeka kwa wakati na kufanya mapitio ya sera, sharia na kanuni.
“Niwaombe wote mliopo hapa kuhakikisha mnatimiza wajibu kwa kutekeleza Programu hii ya ujenzi wa uchumi wa Viwanda ikiwa njia ya uhakika katika kuhakikisha rasilimali za Taifa zinatumika kwa manufaa ya nchi na kuweza kuongeza fursa za ajira kwa Watanzania” alisisitiza Mhagama. 
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (Mb) akizungumza jambo wakati akifungua kikao cha Mawaziri wa Sekta za uchumi walipokutana kujadili utekelezaji wa Programu ya pamoja ya ujenzi wa uchumi wa viwanda katika ukumbi wa mikutano wa Waziri Mkuu Bungeni Jijini Dodoma, Novemba 17, 2018.
????????????????????????????????????
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Joseph Kakunda (Mb) akielezea utekelezaji wa Wizara yake wakati wa kikao hiko walipokutana kujadili utekelezaji wa Programu ya pamoja ya ujenzi wa uchumi wa viwanda, Jijini Dodoma.
????????????????????????????????????
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) akisisitiza jambo wakati wa Kikao hiko cha Mawaziri wa Sekta za kiuchumi walipokutana kujadili utekelezaji wa Programu ya pamoja ya ujenzi wa uchumi wa viwanda, Jijini Dodoma.
????????????????????????????????????
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa (Mb) akielezea umuhimu wa kila Wizara kutekeleza majukumu kwa haraka ili kutimiza malengo wakati wa Kikao hicho.
????????????????????????????????????
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Sekta Binafsi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Ezamo Maponde akiwasilisha mada kwa Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Sekta za Kiuchumi walipokutana Jijini Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...