Na Karama Kenyunko, blogu ya Jamii.


MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeuagiza upande wa mashtaka katika kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili vigogo wawili wa uthamini wa madini ya almasi wa serikali kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kulifuatilia jalada la kesi hiyo na Novemba 17, 2018 wake kueleza maendeleo halisi ya upelelezi dhidi ya kesi hiyo.

Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri ameeleza hayo Leo Novemba 5, 2018 Kesi hiyo ilipokuja kwa kutajwa.Hatua hiyo imekuja baada ya wakili wa serikali, Elizabeth Mkunde kuieleza Mahakama kuwa Kesi hiyo leo ilipangwa kwa ajili ya kutajwa na  upelelezi bado haujakamilika na kwamba DPP ametoa maelekezo ambazo yanafanyiwa Kazi.

Baada ya maelekezo hayo, wakili wa utetezi Nehemiah Nkoko ameeleza kuwa, inaumiza sana, ni mwaka sasa umepita shtaka moja lakini upelelezi wake bado haujakamilika huku dhamana ya washtakiwa ikiwa imezuiwa na kuhoji kuna makesi yenye mashtaka mengi upelelezi wake umekamilika ndani ya miezi mitatu, hili shtaka moja linatimiza mwaka mmoja  unaenda wa pili sasa.

Amedai, shtaka linalowakabili washtakiwa hao, limejitosheleza na lina kila  kitu toka mwaka Jana lugha ni hiyo hiyo upelelezi haujakamilika.Mheshimiwa, tunaamini kiwa DPP  anapozuia dhamana ya mtu basis huyo mtu atasikilizwa kwa wakati, tunaomba Mahakama iwalazimishe upande Wa mashtaka watueleze msimamo halisi wa upelelezi ili tujue wamekwama wapi na sisi tufuatilie." Alieleza Nkoko.

Baada ya kusikiliza hoja zote, Hakimu Mashauri emeutaka upande wa  mashtaka kulifuatilia jalada hilo la kesi. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 17. Mwaka huu.Washtakiwa katika kesi hiyo ni Mkurugenzi wa Uthaminishaji Almasi na Vito Tanzania  (Tansort) Archard Kalugendo na mthamini almasi wa serikali, Edward Rweyemamu ambao ni waajiriwa wa Wizara ya Nishati na Madini,

Kalugendo na Rweyemamu wanasota mahabusu kutokana na DPP kuzuia dhamana zao na Wanakabiliwa na  kesi ya uhujumu uchumi wakidaiwa kuisababishia serikali hasara ya sh 2.4 bilioni.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, washtakiwa wanakabilkiwa na ashtaka la kuisababishia serikali hasara ya sh  2,486,397,982.54 ambapo wanadaiwa kutenda kosa hilo kati ya Agosti 25 na 31, 2017  katika maeneo mbalimbali ya mikoa ya Dar es Salaam na Shinyanga.

Washtakiwa hao wanadaiwa kwa pamoja na kwa vitendo vyao wakiwa wathaminishaji wa almasi wa serikali na waajiriwa wa wizara hiyo waliisababishia serikali hasara ya Dola za Marekani 1,118,291.43  ambazo ni sawa na sh 2,486,397,9.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...