
MBUNGE wa Korogwe vijijini ndugu Timotheo Mnzava, Novemba 18, 2018 amefanya mkutano wake wa kwanza na wananchi mara baada ya kuapishwa rasmi katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma Novemba 6, 2018.
Mkutano huo ambao ulifanyika katika kata ya Makuyuni, Mnzava amewahakikishia wananchi wa jimbo la Korogwe vijijini kutatua kero sugu zilizopo ndani ya jimbo ambapo zile zilizo juu ya uwezo wake kuendelea kuikumbusha serikali kutatua ili wananchi wapate maisha bora.
Aidha Mnzava ameainisha changamoto ya Elimu, Maji, afya na Miundombinu ya barabara ndio vipaumbele ambavyo ataanza kuvishughulikia katika kipindi chake cha kuiongoza Korogwe vijijini.
Mnzava amewahakikishia wananchi kuhusu Korogwe mpya na yenye matokeo chanya inayoenda sambamba na dhamira ya Mh. Rais Dkt John Pombe Magufuli ya kuifikisha Tanzania katika uchumi wa kati ifikapo 2025.
Mnzava alimalizia kwa kumshukuru rais Magufuli, Wananchi pamoja na chama cha mapinduzi kwa imani waliyonayo juu yake na kumchagua kuwa mbunge atakayeiongoza Korogwe vijijini na kuleta maendeleo yenye tija na endelevu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...