-Whozu apanda stejini na Briefcase
lililojaaa mishkaki
-Roma, Stamina waangusha bonge moja
la show
JIJI la Arusha, jana lilishuhudia show za kufunga mwaka
zilizojaa ubunifu na vituko vya aina yake kutoka kwa wasanii mbali mbali waliopanda
jukwaani kutumbuiza kwenye Tamasha la Tigo Fiesta lililofanyilka katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
Msanii Whozu alikuwa ni kivutio kikubwa kutokana na staili
aliyotumia kupanda jukwaani na madensa wake wakiwa wamevalia
nguo za wapishi huku akiwa na
briefcase lililojaa mishkaki.Mashabiki wengi walipigwa na butwaa baada ya kuona Whozu
akifungua briefcase ambalo lilionekana ni la thamani na kutoa mishkati kisha
kutuimbuiza na simbo wa Ita Boda boda Twende Kwa Mromboo ambao ulikuwa ni
kivutioa Whozu na madensa wake, walifanikiwa kuliteka vyema jukwaa
ambapo wakitumbuiza huku wakiwa wanatafuna mishkaki.
Wasanii wengine ambao walifanikiwa kuteka nyoyo za mamia ya
mashabiki waliofurika kwenye tamasha la hilo ni pamoja na Roma, Stamina ambao walipanda
jukwaani pamoja na mwanadada Maua Sama
anayetamba na kibao chake cha Iokote.Wasanii wengine walipanda sjejini ni pamoja na Dogo janja,
Lulu Diva, Rich Mavoko, Fid Q, Weusi na wengine.
Ikiwa ni sehemu ya Vibe la Tigo Fiesta 2018, kampuni ya simu za Simu za
mkononi ya Tigo imewaletea promosheni bab-kubwa inayojulikana ya
Data Kama Lote inayowapa wateja bonasi
ya hadi mara mbili kwa vifurushi vya intaneti watakavyonunua kupitia menu
iliyoboreshwa ya *147*0#.
Tigo pia inatoa punguzo kubwa
la bei kwa tiketi za tamasha la Tigo Fiesta 2018 zitakazonunuliwa kupitia Tigo
Pesa Masterpass QR. Wateja wanapaswa kupiga *150*01# na kuchagua 5 (lipia huduma) kisha kuchagua namba 2
(lipa Masterpass QR) na kutuma kiasi husika cha bei ya tiketi kwenda namba ya Tigo Fiesta 78888888.
Wateja wa Tigo pia wanaweza
kujaribu umahiri wao wa kujibu maswali yanayohusiana na msimu wote wa vibes
kupitia shindano la Tigo Fiesta 2018 –
Chemsha Bongo Trivia. Washindi wanajinyakulia zawadi za kila siku
za TSH 100,000, zawadi za wiki za TSH 1 milioni, simu janja za mkononi zenye
thamani ya TSH 500,000 kila moja, pamoja na donge nono la TSH milioni 10 kwa
mshindi wa jumla.

Msanii Maua Sama anayetamba na kibao chake cha Iokote akitoa burudani
ya aina yake kwa mashabiki wa muziki wa kizazi kipya walioshiriki katika
tamasha la Tigo Fiesta mwaka 2018 lililofanyika katika uwanja Sheikh
Amri Abeid jijini Arusha mwishoni mwa wiki.

Msanii Whozu na madensa wake wakitumbuiza katika Tamasha la Tigo Fiesta 2018 lilofanyika katika kiwanja cha Sheikh Amri Abeid jijini Arusha mwishoni mwa wiki.
Wasanii wanaounda kundi la Weusi wakiongozwa na Joh Makini wakiwapagawisha mamia ya mashabiki walioshiriki katika tamasha la Tigo Fiesta mwaka 2018 lililofanyika katika uwanja Sheikh Amri Abeid jijini Arusha mwishoni mwa wiki.

Rich Mavoko Msanii Rich Mavoko akitoa burudani kwa maimia ya mashabiki waliofurika katika Tamasha la Tigo Fiesta mwaka 2018 lililofanyika katika uwanja Sheikh Amri Abeid jijini Arusha mwishoni mwa wiki.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...