Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
KATIKA kuendeleza mkakati wa kutangaza utalii wa Tanzania
nchini China, Bodi ya Utalii Nchini (TTB) kwa kushirikiana na wadau wa Utalii wa Tanzania
pamoja na Sekta ya Madini inashiriki onesho kubwa la biashara
yaliyoandaliwa na Serikali ya China.
Maonesho hayo makubwa yajulikanayo kama China
International Impact Expo (CIIE) yatafanyika katika jiji la
Shanghai kuanzia 5-10 Novemba, 2018 na Kupitia maonesho
haya, sekta ya madini itaudhihirishia ulimwengu kuwa Madini ya
Tanzanite yanapatikana Tanzania tu.
Akielezea safari hiyo ya nchini China, Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Jaji Mstaafu Thomas Mihayo amesema kuwa safari hiyo ya nchini China imeandaliwa na bodi ya utalii kwa kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania nchini China na Shirika la Ndege la Tanzania ATCL, wameandaa ziara ya utangazaji nchini China ambapo pamoja na
kushiriki maonyesho ya CIIE watafanya ziara ya utangazaji katika
miji mbalimbali.
Amesema miji hiyo ni Shanghai (12 Novemba, 2018), Guangzhou (14
Novemba, 2018), Hong Kong (16 Novemba, 2018), Chengdu (19
Novemba, 2018) na Beijing (20 Novemba, 2018). Misafara hii
itatuwezesha kukutana na wafanyabiashara wa utalii wakubwa
katika miji hiyo na wawekezaji wakubwa katika sekta ya utalii
pamoja na vyombo vya habari mbalimbali vya China.
Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Jaji Mstaafu Thomas akizungumzia safari ya China na ushiriki wao wa Maonesho makubwa yajulikanayo kama China International Impact Expo (CIIE) yatafanyika katika jiji la Shanghai kuanzia 5-10 Novemba, 2018, Kushoto ni Mihayo Meneja Masoko na Usambazaji Edward Mkwabi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...