Na David Nyembe, Chunya 

MKUU wa Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya, Maryprisca Mahundi, amewapa wiki tatu wafugaji wa Kijiji cha Igundu katika Kata ya Sangambi wilayani humo kuhamisha mifugo yao na kuipeleka katika Kijiji cha Paris ambacho kimetengwa kwa ajili ya wafugaji.

Ametoa kauli hiyo wakati wa Mkutano wa Hadhara uliofanyika kijijini hapo ambapo alisema lengo la kuondoa mifugo hiyo ni kumaliza mgogoro kati ya wakulima wa kijiji hicho na wafugaji pamoja na kuokoa chanzo cha maji ambacho wakazi wa eneo hilo wanakitegemea. Alimuagiza Ofisa Mtendaji wa Kijiji hicho, Joseph Nangale, kusimamia na kuhakikisha mifugo hiyo inahamishwa huku akimtaka kutumia nguvu iliyotumika kuwazuia wakulima kufanya shughuli zao karibu na chanzo cha maji.

Mahundi alisema amechoshwa na migogoro ya wakulima na wafugaji katika kijji hicho cha Igundu na kwamba agizo lake hilo ni la mwisho na kwamba atakaporudi tena kwenye kijiji hicho na kukuta inaendelea hakutakuwa na majadiliano tena na kwamba wasije wakamlaumu.

“Mkae chini mjadiliane na mkubaliane idadi ya mifugo ambayo kila mfugaji wa kijiji hiki atatakiwa kubaki nayo hapa, nimewapa siku 10 viongozi wenu waniletee taarifa ya majidiriano hayo, lakini nimewashauri kila mfugaji abaki na mifugo 10,” alisema Mahundi.

Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya Meryprisca Mahundi (katikati) akimkisikiliza kwa makini Afisa Mtendaji Kata ya Sangambi kijiji cha Igundu  Joseph Nangale ,kuhusiana na namna ambavyo wafugaji wamefanya uhalibifu wa vyanzo vya maji katika kjiji hicho.Picha David Nyembe . 
Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mh Meryprisca Mahundi (Katikati)akiteta jambo na viongozi wa vijiji vinavyo zunguka kata ya Sangambi ambako kumefanyika uhalibifu wa vyanzo vya maji kutokana na baadhi ya wafugaji wa vijiji hivyo kunywesha mifugo yao sanjali na kupitisha mifugo katika maeneo ya vyazno hivyo. 
Wananchi wa kijiji cha Igundu wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Chunya Merryprisca Mahundi (hayupo pichani) mara baada ya kukamilisha ziara ya  kutembelea maeneo ya vyanzo vya maji ambako kumefanyika uhalibifu mkubwa kutokana na baadhi ya wafugaji kupitisha mifugo yao .


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...