Na Mwandishi Wetu
KATIBU Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Leonard Akwilapo ameshukuru Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi Elimu na Utamaduni (UNESCO) na Ubalozi wa Korea Kusini kwa kufanikisha warsha inayoandaa mpango kazi kwa walimu na wadau wanaosimamia mafunzo ya ufundi stadi.
Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya mradi wa Bear ll Katibu Mkuu huyo alisema wakati taifa linaelekea katika uchumi wa viwanda mradi huo na mafunzo yake ni kitu muhimu sana.
Mafunzo hayo ya siku tatu yalijadili namna ya kufikisha elimu ya ufundi stadi inayooana na mahitaji halisi ya nguvu kazi katika jamii.
Mafunzo hayo yalilenga kutambua na kusaidia kufanikisha malengo matatu ya matumizi ya ufundi stadi yanayozingatia mahitaji ya uchumi, kuboresha mafunzo  ya ufundi stadi kwa wateja na kuboresha hali ya uelewa wa ufundi stadi miongoni mwa vijana na wananchi.
Katibu mkuu huyo alisema kwamba serikali inajivunia hatua iliyofikiwa ya mradi huo wa Bear ll ya uandazi wa mpango kazi wa mwaka mmoja na wa miaka mitatu ambao kwa sasa unasubiri kamati ya wizara kuupitia na kuubariki.
Alisema kwamba Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia itahakikisha kwamba mradi huo wa Bear ll unatekelezwa na kutoa matunda yanayotarajiwa.
Katika warsha hiyo mada kadhaa ziliwasilishwa ikiwamo mkakati wa UNESCO kuhusu ufundi stadi na historia ya mradi wa Bear II ambao unapoletwa  nchini Tanzania upo katika awamu ya pili.
Mradi huo wa Bear ll unafanyika katika nchi tano zikiwamo Tanzania na Uganda katika awamu yake ya pili. Nchi zingine ni Ethiopia, Kenya na Madagascar.
Kwa mujibu wa taarifa za kitafiti kuna malalamiko kwamba wahitimu wa ufundi stadi wanashindwa kwenda sanjari na matakwa ya shughuli zao katika viwanda.
 Mkuu wa kitengo cha Elimu katika shirika la UNESCO, Bi. Faith Shayo akitoa neno la ukaribisho kwa meza kuu na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Leonard Akwilapo wakati wa kufunga mafunzo ya mradi wa Bear ll na warsha ya kiufundi yaliyofanyika katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Dk. Noel Mbonde akizungumzia mradi wa BEAR II kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Leonard Akwilapo kufunga mafunzo ya mradi wa Bear ll na warsha ya kiufundi yaliyofanyika katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Leonard Akwilapo akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya mradi wa Bear ll na warsha ya kiufundi yaliyofanyika katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
 Ofisa Balozi mdogo wa Ubalozi wa Korea nchini, Bi. Jiin An akitoa salamu za serikali ya Korea Kusini kwa niaba ya Balozi wa Korea Kusini, Mh. Geum Young Song wakati wa kufunga mafunzo ya mradi wa Bear ll na warsha ya kiufundi yaliyofanyika katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
 Mratibu wa mradi wa BEAR II kutoka ofisi za Unesco Nairobi, Bw.Teeluck Bhuwanee akitoa neno kwa niaba ya Unesco wakati wa kufunga mafunzo ya mradi wa Bear ll na warsha ya kiufundi yaliyofanyika katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau kutoka MoEST, Wizara wa Kilimo, UNESCO, NACTE, TCCA, ATE, VETA pamoja wadau wa maendeleo walioshiriki halfa ya kufunga mafunzo ya siku tatu ya mradi wa Bear ll na warsha ya kiufundi yaliyofanyika katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Leonard Akwilapo pamoja na washiriki wakati wa kufunga  mafunzo ya mradi wa BEAR ll na warsha ya kiufundi yaliyofanyika katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye picha ya pamoja. BEAR ll ni mradi wenye lengo la kuleta elimu bora kwa mataifa ya Afrika
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...