Na Dotto Mwaibale, Kisarawe

VIKUNDI vya wakulima 750 vya Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani vinatarajia kukabidhiwa hati miliki za ardhi zitakazoweza kuwasaidia kupata mikopo katika taasisi za fedha.

Hayo yalibainika wilayani humo juzi katika Kijiji cha Zegero wakati wa mkutano wa mchakato wa kuanzisha jukwaa la wakulima unaoratibiwa na Shirika la The Winamwanga Cultural Heritage Association kwa kushirikiana na Ofisi ya mkurugenzi wa halmshauri hiyo.

Akizungumza katika mkutano huo Ofisa miradi wa shirika hilo, Said Simkonda alisema kati ya vikundi hivyo vitakavyopata hati hizo vikundi 250 ni vya watu wenye ulemavu ambavyo vimepata mashamba kwa ajili ya kufanya kilimo.Akizungumzia kuhusu uanzishwaji wa jukwaa la wakulima alisema litakuwa ni chombo cha kuwakutanisha wakulima wote waliomo wilayani Kisarawe na mikoa ya jirani ili kuleta kilimo chenye tija.

Alisema mchakato huo umewahusisha wadau wa kilimo kutoka Kata ya Kurui, Mzenga, Mafizi, Vihingo, Marui na Chole na kuwa shirika hilo linaupongeza uongozi wa Halmshauri ya Wilaya ya Kisarawe kwa kulidhia kuupokea mradi huo wa kilimo mnamo mwaka 2016.
Ofisa Miradi wa Shirika la The Winamwanga Cultural Heritage Association, Saidi Simkonda, akizungumza na wadau wa kilimo ambao ni wanachama wa shirika hilo kuhusu mchakato wa uanzishwaji wa Jukwaa la Wakulima wilayani Kisarawe mkoani Pwani pamoja na kukabidhiwa hati miliki za ardhi. Kushoto kwake ni Diwani wa Kata ya Kurui, Musa Kunikuni.
`Ofisa Ardhi wa Shirika la The Winamwanga Cultural Heritage Association, Ivy Jamson Mwansepe, akitoa taarifa ya shirika hilo wakati wa mkutano huo.
Ofisa Ardhi wa Shirika la The Winamwanga Cultural Heritage Association, Ivy Jamson Mwansepe, akimkabidhi taarifa hiyo Diwani wa Kata ya Kurui, Musa Kunikuni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...