Na Stella Kalinga, Simiyu
Wafanyabiashara kutoka nchini Uturuki wameonesha nia na dhamira ya kuwekeza katika ujenzi wa kiwanda cha kutengeneza nguo mkoani Simiyu ambacho kitakuwa na uwezo wa kuajiri watu zaidi ya 4000.

 Hayo yamebainishwa katika kikao kati ya Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo ambaye aliambatana na Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara na mwakilishi wa Wafanyabiashara wa Uturuki kutoka makampuni saba ya nchi hiyo, katika kikao maalum na viongozi wa Mkoa wa Simiyu, Wakuu wa Taasisi mbalimbali na jumuiya ya wafanyabiashara ya mkoa wa Simiyu, kilichofanyika Novemba 22, 2018 Mjini Bariadi.

Balozi Kiondo amesema Wafanyabiashara hao wanayo azma ya kuwekeza katika kiwanda cha kutengeneza nguo katika mnyororo mzima wa utengenezaji kutoka bidhaa ya awali ya pamba mpaka bidhaa ya mwisho kabisa, ambayo ni nguo kwa ubia(partineship) na Watanzania.

Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara kutoka Uturuki, Bw. Cengiz ERTAS amesema  mpaka sasa ni makampuni sita kutoka nchini humo yameonesha nia ya kuwekeza katika kiwanda cha nguo mkoani Simiyu na akaahidi kwenda kuwashawishi wafanyabiashara wenzake hivyo watakaporudi kwa mara nyingine  makapuni mengi yatakuja kuwekeza katika viwanda vya nguo.

“Nikirudi nyumbani kama kiongozi wa wafanyabiashara nitawashawishi wengine pia waje wawekeze katika viwanda vya nguo,ombi langu kwenu ni kwamba ninahitaji Mfanyabiashara Mtanzania ambaye tutashirikiana naye katika uwekezaji huu(partinership), lakini niwahakikishie tu kuwa katika kiwanda tutakachojenga mashine na vifaa vyote vipo tayari kule Uturuki” alisema  Cengiz.
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza katika kikao cha viongozi wa Mkoa wa Simiyu, baadhi ya viongozi wa Taasisi za Serikali, Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo na Mwenyekiti na mwakilishi wa Wafanyabiashara kutoka Uturuki, Bw. Cengiz ERTAS,  kilichofanyika Novemba 22, 2018 Mjini Bariadi.
 Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo akizungumza viongozi wa Mkoa wa Simiyu, baadhi ya viongozi wa Taasisi za Serikali katika kikao kilichofanyika Novemba 22, 2018 Mjini Bariadi kwa lengo la kujadili uwekezaji katika viwanda vya nguo unaotarajiwa kufanywa na Wafanyabiashara kutoka nchini Uturuki katika mkoa wa Simiyu.
 Mwenyekiti na mwakilishi wa Wafanyabiashara kutoka Uturuki, Bw. Cengiz ERTAS, akizungumza na viongozi wa Mkoa wa Simiyu, baadhi ya viongozi wa Taasisi za Serikali, Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo katika kikao kilichofanyika Novemba 22, 2018 Mjini Bariadi.
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Mkoa wa Simiyu ambaye pia ni Mbunge wa Itilima, Mhe. Njalu Silanga akichangia hoja katika viongozi wa Mkoa wa Simiyu, baadhi ya viongozi wa Taasisi za Serikali, Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo na Mwenyekiti na mwakilishi wa Wafanyabiashara kutoka Uturuki, Bw. Cengiz ERTAS,  kilichofanyika Novemba 22, 2018 Mjini Bariadi kwa lengo la kujadili uwekezaji katika viwanda vya nguo mkoani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (wa tatu kushoto)  akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo(wa pili kushoto), na Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara na  mwakilishi wa Wafanyabiashara kutoka Uturuki, Bw. Cengiz ERTAS( wa tatu kulia),  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Edwin Mhede( wa pili kulia) na viongozi wa Serikali pamoja na wafanyabiashara wa mkoa huo, mara baada ya kuhitimisha kikao mjini Bariadi kilichofanyika kujadili uwekezaji katika viwanda vya nguo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...