NA MWAMVUA MWINYI, PWANI 

WATU sita kati yao akiwemo mtoto mchanga jinsia ya kike ,waliofariki dunia katika ajali ,iliyotokea kijiji cha Msata, barabara kuu ya Segera /Chalinze mkoani Pwani ,wametambuliwa majina yao ili ndugu wakabidhiwe kwa ajili ya mazishi. 

Akitoa taarifa za muendelezo kuhusu ajali hiyo, kamanda wa polisi mkoani Pwani, (ACP) Wankyo Nyigesa alisema hakuna idadi ya vifo iliyoongezeka zaidi ya taarifa iliyotolewa awali. Alitaja miili ya marehemu iliyotambuliwa kuwa ni Ibrahim Kilama (28), Mohammed Amir Shekaoneka (28 mkazi wa Korogwe na Omary Rashid (28) Tanesco Magomeni jijini Dar es salaam. 

Wengine ni Lihatu Yahaya mtoto mchanga miezi mitatu mkazi wa Handeni ,Hassan Zabuni kondakta wa gari namba T. 124 DHW aina ya Toyota coaster na Emmanuel Cosmas (30) mkazi wa Chalinze . Aidha Wankyo alieleza, watu saba waliopata majeraha kwenye maeneo mbalimbali ya mwili yao , kati yao watano wameruhusiwa baada ya kupatiwa matibabu na wengine wawili bado wapo hospital ya Tumbi Kibaha kwa ajili ya matibabu zaidi. 

“Ajali hiyo ilitokea novemba 5, majira ya saa moja usiku baada ya gari namba T. 124 DHW aina ya Toyota coaster ikitokea Mkata kwenda Mbezi -Dar es salaam ,kuligonga kwa nyuma bila kuchukua tahadhari ,lori namba KBV 746C/ZE2861 FAW iliyokuwa imeegeshwa barabarani kutokana na kuharibika.” Wankyo alitaja chanzo cha ajali, ni uzembe wa dereva wa gari namba T. 124 DHW aina ya Toyota coaster kujaribu kulipita bila tahadhari gari jingine lililokuwa limeegeshwa baada ya kuharibika na wanaendelea kumsaka. 

Kamanda huyo alitoa rai kwa madereva, kutii sheria za usalama barabarani na kudai hawatakuwa na muhali nao wale watakaokiuka sheria ili iwe fundisho kwa wengine.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...