NA MWAMVUA MWINYI,CHALINZE

WODI ya uzazi katika kituo cha afya Chalinze,mkoani Pwani inakabiliwa na baadhi ya changamoto ikiwepo ufinyu wa jengo hali inayosababisha wakati mwingine akinamama wazazi kusongamana na kulazimika kulala wawili katika kitanda kimoja.

Aidha kina tatizo jingine la upungufu wa vitanda na watumishi wa afya hasa madaktari . Akikabidhiwa msaada wa vifaa vya akinamama waliojifungua kutoka kwa kikundi cha Pwani generation queens ,mganga mfawidhi wa kituo hicho Salama Masukuzi alisema kuwepo kwa mlundikano wa wagonjwa kunatokana na upungufu wa majengo ya wodi ya uzazi pamoja na vitanda .

Alieleza ,kwasasa wapo maafisa tabibu wanne ,madaktari wasaidizi wawili na daktari mmoja ambao bado ni wachache kutekeleza majukumu yao ya kutoa huduma bora ya kiafya . “Kituo hiki kinapokea wagonjwa mbalimbali na wengine wakitokea kwenye zahanati 44 zinazozunguka halmashauri ya Chalinze suala ambalo linawawia vigumu kutekeleza wajibu wao ” alifafanua Salama .

Alieleza wamepata manesi wanne kupitia ajira mpya, ameishukuru serikali lakini aliiomba kuwaboreshea zaidi huduma ya afya ili kuwahudumia wananchi. Kwa upande wa akinamama wa Chalinze,akiwemo Demertia Milichadesi pamoja na Mariam Muhoja walisema wanapata shida katika kununua drip,vifaa vya uzazi na kipimo cha kujua wingi wa damu ambacho hutakiwa kwenda nje wakati mjamzito akiwa tayari yupo wodini.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...