Na Karama Kenyunko, Blogu ya Jamii.

MUIGIZAJI maarufu wa filamu Tanzania Wema Sepetu amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Novemba Mosi, 2018, akikabiliwa na shtaka moja la kuchapisha picha za ngono mtandaoni.

Wema ambaye pia ni Miss Tanzania mwaka 2006, anashtakiwa chini ya kifungu cha sheria namba 14(1)(b) na( 2) (b) cha makosa ya mtandao.Akisoma hati ya mashtaka, Wakili wa Serikali Mwanaamina Kombakono amedai mbele ya Hakimu Mkazi Maira Kasonde kuwa  Oktoba 15, 2018, katika maeneo tofauti tofauti jijini Wema kupitia 
ukurasa wake wa Instagram alichapisha picha za ya video za ngono ( Phonograph).

Hata hivyo, Wema ambaye alitinga kizimbani saa saba kasorobo mchana amekana kutenda kosa hilo.Wakili anayemtetea Wema, Simwanza Rubeni ameiomba Mahakama kumpatia mteja wake dhamana kwa kuwa shtaka linalomkabili mshtakiwa Wema 
linadhaminika.

Pia ameiomba Mahakama kumpatia mteja wake huyo masharti nafuu 
ya dhamana.Hata Wakili Kombakono alipinga na kuiomba mahakama kumpatia mshtakiwa huyo masharti magumu ya dhamana kwani kitendo alichofanya kijamii na kimaadili linapingana kabisa na maadili ya Tanzania, amedai mshtakiwa Wema pia anafollowers wengi sana kwenye ukurasa wake wakiwemo watoto wadogo ambao wanakuwa wanafuatilia kile anachofanya.

"Tunaomba mahakama ikiwezekana iweke masharti magumu kwake ili iwe fundisho kwa wale ambao wangependa kuiga,"amesema Wakili.Hata hivyo Wema yuko nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana.Mahakama imemtaka Wema mwenyewe kisaini bondi ya sh. Milioni 10 na kuwa na mdhamini mmoja ambaye atakayesaini bondi ya kiasi hicho cha fedha.

Pia Mahakama imempiga marufuku mshtakiwa Wema kutochapisha picha yoyote ya ngono katika ukurasa wake wa Instagram au kuchapisha maneno yoyote yenye viashiria vya ngono.Kesi hiyo  imeahirishwa hadi Novemba 20.2018 Kwa mujibu wa upande wa 
mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...