Na Balthazar Mashaka, Mwanza
MMOJA wa askari watano waliotunukiwa vyeo na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro, kutokana na utendaji wao amesema kuwa alinusurika kupigwa risasi na jambazi wakati wakijiandaa kuwakabili katika eneo la Nyegezi,jijini Mwanza.
Askari huyo WP 12415 Dominica Michael Nnko ambaye ametunukiwa cheo cha Koplo alisema kuwa Februari 2017, alinususurika kuuawa kwa kupigwa risasi baada ya kuwahiwa na jambazi lakini kwa ujasiri alitumia mbinu ya uaskari kuwahi kulala chini kabla jambazi huyo kufariki kwa kupigwa risasi na askari wenzake.
Koplo Michael alieleza kuwa usiku wa siku ya tukio hilo laambayo ilikuwa siku ya kuzaliwa kwake, walipangwa kuwakabili majambazi huko Nyegezi, kumbe eneo walikopangwa aliwahiwa na jambazi mmoja bila kumuona ambaye alimlenga kwa bunduki.
“Kwanza nashukuru kwa kupata cheo hiki ambacho sikukitarajia ambacho kinatokana na viongozi kutambua mchango wangu katika kulinda usalama wa raia na mali zao.
"Maishani mwangu sitasahau tukio la Februari 19, 2017 ambayo ilikuwa siku ya kuzaliwa kwangu. Nilinusurika kuuawa nikiwa kazini,” alisema Koplo Michael.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Jonathan Shanna akimvisha cheo Konstebo WP. 12415 Dominica Michael Nnko cheo kuwa Koplo kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro baada ya kuwatunukia vyeo hivyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...