*Mkurugenzi Mtendaji Mkuu atangaza uhakiki wa wafanyakazi nchi nzima
*Azungumzia kuanza kufanya tafiti kubaini wasomaji,wasikilizaji wa vyombo vyao
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
MKURUGENZI Mtendaji Mkuu wa Uhuru Media Group ambayo inasimamia vyombo vya habari vya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Ernest Sungura ameamua kuwapa motisha wafanyakazi wote wa kampuni hiyo kama sehemu ya kuthamini mchango wao.
Amesema motisha hiyo inakwenda sambamba na uhakiki wa wafanyakazi wote wa kampuni hiyo huku akielezea namna ambavyo amefurahishwa na utendaji kazi wa wafanyakazi wote na hasa katika kumuunga mkono Rais Dk.John Magufuli ambaye amefanya mambo makubwa kwa mwaka 2018.
Akizungumza leo ofisini kwake Sungura amesema Desemba 28 mwaka huu wa 2018 amekutana na wafanyakazi wote kwa kada mbalimbali na alitumia sehemu hiyo kuelezea mikakati ya kampuni hiyo ambayo imedhamiria kufanya mambo makubwa.

"Tulipokutana
na wafanyakazi kuna mambo mengi ambayo tumeyazungumza.Pia nilitumia
nafasi hiyo kuwashukuru kwa kumuunga mkono Rais Magufuli kwa kazi nzuri
anayofanya. Rais wetu amefanya mambo makubwa kwa mwaka huu yakiwamo ya
kuboresha sekta ya anga, miundombinu kwa upanuzi wa barabara na ujenzi
wa madaraja, umeme wa mto Rufiji ,ununuzi wa korosho, elimu bure na
mambo mengine mengi ambayo yamefanyika.Hivyo wafanyakazi hawa wamekuwa
wakiunga mkono kwa vitendo jitihada za Rais,"amefafanua.
Ameongeza wafanyakazi wa Uhuru Media Group kwa mwaka huu wa 2018 wamefanya kazi kwa bidii, hivyo ameamua kuwapongeza kwa kuwapa motisha kwani kesho ni Januari moja ni vema wakauanza mwaka vizuri."Kila mfanyakazi aliyeajiriwa na wasioajiriwa lakini wanafanya kazi kwenye vyombo vya habari vya chama tutawapa motisha hiyo.Tutafanya kwa walioko Dar es Salaam na wa mikoani," amesisitiza.
Aidha mbali ya kutoa motisha atatumia nafasi hiyo kufanya uhakiki wa wafanyakazi waliopo kwenye vyombo hivyo na iwapo kutakuwa na wafanyakazi hewa atawabaini."Nataka kumuona kila mfanyakazi uso kwa uso .Rais wetu aliamua kufanya uhakiki kwa watumishi wa Serikali ,nami namuunga mkono kwa kufanya uhakiki wa wafanyakazi wetu."amesema Sungura.

MKURUGENZI
Mtendaji Mkuu wa Uhuru Media Group ambayo inasimamia vyombo vya habari
vya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ernest Sungura akifafanua jambo
alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini
Dar kuhusu mambo mbalimbali ikiwemo kuwapa motisha wafanyakazi wote wa
kampuni hiyo kama sehemu ya kuthamini mchango wao,aidha mbali
ya kutoa motisha atatumia nafasi hiyo kufanya uhakiki wa wafanyakazi
waliopo kwenye vyombo hivyo na iwapo kutakuwa na wafanyakazi hewa
atawabaini na kuchukua hatua.
MKURUGENZI
Mtendaji Mkuu wa Uhuru Media Group Ernest Sungura akielezea mbele ya
Waandishi wa habari leo Ofisini kwake jijini Dar,namna kampuni hiyo
inavyojipanga ,amesema
kuanzia mwakani wataanza kufanya utafiti
utakaochukua muda wa miezi mitatu na lengo ni kufahamu wasomaji
wao,wasikilizaji wao na watazamaji wao wanataka nini."Pia Februari mwaka
2019 tutafanya 'uzinduzi laini' wa vyombo vyetu na Aprili 2019 tutafanya
uzinduzi rasmi,ambapo ndio tutazungumza malengo na mikakati
yetu.",alifafanua Sungura.
MKURUGENZI
Mtendaji Mkuu wa Uhuru Media Group Ernest Sungura akimkabidhi mmoja
wa wafanyakazi kutoka Idara ya Utawala, Banga Lucas kiasi cha fedha ikiwa
ni sehemu ya motisha iliyotolewa kwa wafanyakazi wote wa kampuni hiyo
ikiwa kama sehemu ya kuthamini mchango wao.Picha na Michuzi Jr-MMG.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...