Askofu Mkuu wa Kanisa la Africa Inland Church Tanzania (AICT) Dayosisi ya Mwanza, Askofu Philipo Magwano (pichani) hii leo Disemba 23, 2018 amewekwa wakfu na kusimikwa kazini katika ibada maalum iliyoongozwa na Askofu Mkuu wa kanisa hilo nchini, Askofu Mussa Magwesela katika kanisa la AICT Makongoro Jijini Mwanza.
Jopo la Maaskofu wa Kanisa la AICT wakimweka wakfu na kumsimika kazini Askofu Mkuu wa Kanisa la Africa Inland Church Tanzania (AICT) Dayosisi ya Mwanza, Askofu Philipo Magwano.
Mgeni rasmi kwenye ibada hii maalum ya kumweka wakfu na kumsimika kazini Askofu Mkuu Kanisa la AICT Dayosisi ya Mwanza alikuwa Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (wa pili kushoto).Tazama BMG Online TV hapa chini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...