*Ni baada ya kusambaza taarifa ya kuruhusiwa kufanya maonesho nje ya nchi.


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA) limewaonya wasanii kutoka kundi la WCB   Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz 'na Msanii mwenzake Raymond Mwakyusa 'Rayvan' kuacha kusambaza taarifa za uongo.

Taarifa hiyo imetolewa na Katibu Mtendaji wa BASATA Onesmo Kayanda baada ya wasanii hao kutoa kauli jana ya kuruhusiwa kufanya maonesho nje ya nchi baada ya kuwaandikia barua baraza na kuwaomba na wakawaruhusu.

Baraza limekanusha habari zinazosambaa kwenye vyombo vya habari hususani mitandao ya kijamii kuwa limewaruhusu Diamond na Rayvan.

Mnamo Desemba 18 2018, Baraza liliwafungia wasanii hao kutokujiahughulisha na sanaa ndani na nje ya nchi kwa kipindi kisichojulikana kutokana na kutumia kwa makusudi wimbo wa Mwanza ambao umefungiwa kwa sababu za kimaadili.

Baraza limeendelea kusisitiza kuwa halijawafungulia wasanii hao Diamond na Rayvan kufanya onesho lolote la sanaa ndani na nje ya nchi.

Aidha, baraza kwa mara nyingine linawataka wasaii hao kutii maagizo waliyopewa na kuacha mara moja kupotosha umma kwa kusambaza taarifa za uongo kabla ya hatua kali zaidi kuchukuliwa dhidi yao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...