Na Vero Ignatus,Kilimanjaro.

Mafunzo yametolewa kwa Maafisa Ugani 30 kutoka katika kata mbali mbali za wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro kujua kanuni bora za kilimo cha kahawa yatakayosaidia kufufua zao hilo na kuhamasisha kilimo cha zao hilo ili kukuza pato la mkoa huo na taifa kwa ujumla.

Dafrosa Sanga ni Meneja Uendeshaji wa Shirika la Cafe Africa lililoendesha Mafunzo hayo amesema kuwa wameamua kujikita katika zao la kahawa kwani ni moja kati ya mazao yaliyopewa kipaumbele na serikali ikiwemo Korosho,pamba na chai.Dafrosa amesema kuwa mafunzo hayo huendeshwa kwa vitendo kuanzia kwenye kutesha miche,kuvuna na mnyororo wa thamani ili Maafisa Ugani hao waweze kuwasaidia wakulima kuboresha kilimo cha kahawa.

Kipi Warioba ni Mkuu wa Wilaya ya Moshi amewataka Maafisa Ugani hao wasikae Maofisini bali waende kupeleka ujuzi na marifa waliyoyapata kwa wakulima ili kuongeza uzalishaji wa kahawa kwani uchumi wa mkoa huo umekua ukitegemea zao hilo kwa miaka mingi.Warioba alisema kuwa soko la kahawa la dunia bado linafanya vizuri hususan kwa kahawa bora imekua ikipata bei nzuri ukilinganisha na kahawa isiyokua na ubora imekua ikipata bei ya chini.

Mwakilishi wa Mafisa Ugani hao Magnus Mwang`ata alisema kuwa wanatarajia kuandaa mpango kazi pamoja na kuwa na mashamba darasa kila kata ili kuweza kuwaelimisha wakulima juu ya kilimo bora cha kahawa kitakachowasaidia kuinua pato la mkulima.

Magnus alisema kuwa Mafunzo hayo yamewasaidia kuongeza mbinu mpya za kilimo cha kahawa kwani teknolojia hubadlika kadiri miaka inavyokwenda hivyo ushirikiano wa Cafe Africa na Jukwaa la Wadau wa Kahawa (ANSAF) utawajengea uwezo Maafisa hao kukuza zao la kahawa.

Mkuu wa Wilaya ya Moshi Kipi Warioba akiotesha Kahawa katika shamba darasa katika kijiji cha Mwasi Kusini

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...