Na Andrew Chale, BAGAMOYO
MWANAMUZIKI nguli wa miondoko ya Afro reggae, Jhikolabwino Manyika maarufu Jhikoman kwa kushirikiana na Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) Ijumaa ya 14 Desemba, 2018, amezindua rasmi albam yenye nyimbo sita tukio lililofanyika mjini Bagamoyo,Mkoani Pwani.

Jhikoman  ambaye anatoka kwenye lebo ya AfriKabisa ameweza kuonesha ukongwe  katika muziki huo kwa kufanya kazi pamoja na vijana wadogo ambao ni wanafunzi wa Chuo cha Sanaa TaSUBa  na kukonga nyoyo mashabiki waliojitokeza kwa wingi kwenye uzinduzi huo.

Albam hiyo ina beba nyimbo kama: Mara ya kwanza, Ndotoni, Safari, Bad mind,Time to love na Kuagana zilizo kwenye mtindo wa regge.

Katika uzinduzi huo, Msanii Vitalisi Maembe na wengine wakiwemo Sinaubi Zawose, Voice of Revolution, K’Gwana Shija pamoja na Bocka T waliwez kupamba jukwaa katika kusindikiza uzinduzi huo kwa kuimba nyimbo zao mbalimbali.

Jhikoman ameshukuru uongozi wa TaSUBa kwa ushirikiano  wa kutayarisha albam na kuirekodi kupitia studio ya chuo hicho.

“Wasanii waliopiga vyombo na kuimba na mimi hapa jukwaani  ndio nilioshirikiana nao katika albam hii ni wa TaSUBa. Nashukuru kwa Uongozi kuwapa fursa ya kufanya kazi hii. Lakini pia nawashukuru Watanzania kuendelea kutuunga mkoni katika kazi zetu na kwa sasa albam itakuwa inapatikana pale Afrikakabisa hapa Bagamoyo na maeneo mengine tutaendelea kuwatangazia” alieleza Jhikoman.

Na kuongeza albam hiyo imebeba ujumbe mbalimbali  hivyo itakuwa inaburudisha na pia kufundisha Jamii.

Msanii Jhikoman wa Afrikabisa akishirikiana na Wanafunzi wa TaSUBa wakiimba baadhi ya nyimbo zilizopo kwenye albam ndogo ya Safari ya Gitaa Baridi iliyoandaliwa kwa ushirikiano wa TaSUBa na Afrikabisa wakati wa uzinduzi huo Usiku wa Ijumaa ya 14 Desemba 2018. 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...