Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza, Stanslaus Mabula (CCM) ametoa shilingi Milioni 22 kwa ajili ya ujenzi wa sehemu ya soko la Mlango Mmoja iliyoteketea kwa moto miezi mitatu iliyopita. Mabula aliyasema hayo jana baada ya kuwatembelea wafanyabiashara wadogo (machinga) katika soko hilo na kubainisha kwamba fedha hizo kutoka mfuko wa jimbo zitasaidia ujenzi wa paa lote.

Mwenyekiti wa soko hilo, Jackson Kayoza alisema kulingana na tathmini iliyofanyika, shilingi Milioni 98 zinahitaji kwa ajili ya ujenzi wa sehemu iliyoungua moto hivyo alimshukru mbunge Mabula kwa mchango huo. Mmoja wa machinga katika Soko la Mlango Mmoja ambaye pia bidhaa zake zilitekeketea kwa moto, Isaack Julius, alisema mchango wa mbunge Mabula uwe chachu kwa Halmashauri ya Jiji la Mwanza kwa kuhakikisha inakamilisha kiasi cha fedha kinachohitajika ili ujenzi huo uanze mara moja.

Septemba 28, 2018 majira ya alfajiri, ajali ya moto ilizuka katika Soko la Mlango Mmoja na kusababisha meza 83 za wajasiriamali, maduka 23 na vyoo vitatu kuteketea ambapo hasara yake haikujulikana mara moja.
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula (katikati), akizungumza na wafanyabiashara wadogo (machinga) katika Soko la Mlango Mmoja Jijini Mwanza.
Tazama BMG Online TV hapa chini

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...