Mkutano kati ya Tanzania na Uganda kujadili namna ya kuimairisha mahusiano ya kibiashara na kiuchumi ulifanyika Mutukula, Uganda kuanzia tarehe 17 hadi 19 Desemba 2018. Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Joseph Kakunda na Waziri wa Viwanda, Biashara na Ushirika wa Uganda, Mhe. Amelia Kyabambadde waliongoza ujumbe wa nchi zao katika mkutano huo.
Mkutano huo ulihitimishwa kwa Mawaziri kusaini taarifa ya makubaliano ambayo pamoja na mambo mengine, waliafikiana kuvitafutia ufumbuzi vikwazo vya kibishara na vile visivyo vya kiforodha vinavyozorotesha biashara baina ya nchi hizo mbili.
Mkutano huo ulianza kwa ngazi ya Wataalamu na Makatibu Wakuu ambapo ujumbe wa Tanzania uliongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Joseph R. Buchwaishaija.
Aidha, Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Mhe. Dkt Aziz Ponary Mlima na Balozi wa Uganda nchini Tanzania, Mhe. Richard Kabonero walishiriki mkutano huo.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Mutukula, Uganda
Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Joseph Kakunda (kulia) na
Waziri wa Viwanda, Biashara na Ushirika wa Uganda, Mhe. Amelia
Kyabambadde wakibadilishana taarifa ya mkutano kati ya Tanzania na
Uganda uliojadili namna ya kuimarisha biashara na kuondoa vikwazo vya
kibiashara na visivyokuwa vya kiforodha uliofanyika Mutukula, Uganda
tarehe 19 Desemba 2018.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...