MBUNGE wa Ilala, Mussa Azzan Zungu amezinduwa rasmi kampeni ya Mkoa kwa Mkoa, Rudi Nyumbani Kumenoga inayoendeshwa na Shirika la Mawasiliano Tanzania-TTCL Corporation ikiwa ni kuhamasisha uzalendo kumuunga mkono Rais wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli kauli ya Juni 21, 2018 alipokuwa akipokea gawio la Tsh Bilioni moja na nusu kutoka TTCL Corporation.

Mbunge Zungu aliwataka wananchi wa Ilala kutumia huduma za TTCL ili kukuza uchumi wa Tanzania moja kwa moja kutokana na faida zinazopatikana kutumika kuleta maendeleo kwa jamii.

Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan Zungu (katikati) akionesha bango kuashiria uzinduzi rasmi wa kampeni ya Mkoa kwa Mkoa, Rudi Nyumbani Kumenoga katika wilaya hiyo usiku huu. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba pamoja na mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Ilala (kulia).

Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan Zungu akizungumza kwenye uzinduzi rasmi wa kampeni ya Mkoa kwa Mkoa, Rudi Nyumbani Kumenoga katika wilaya ya Ilala kuhamashisha matumizi ya huduma na bidhaa za Shirika la TTCL.

Baadhi ya wacheza shoo wakiwaburudisha wananchi waliojitokeza katika uzinduzi huo.

Shishi Baby aka Shilole akikimbiza katika kampeni hizo zilizofanyika uwanja wa Karume.


Msanii nguli Dully Skykes akiwapagawisha mashabiki wake katika kampeni ya Mkoa kwa Mkoa, Rudi Nyumbani Kumenoga, Wilaya ya Ilala.
 
Sehemu ya wananchi waliojitokeza kwenye uzinduzi rasmi wa kampeni ya Mkoa kwa Mkoa, Rudi Nyumbani Kumenoga katika wilaya ya Ilala, Uwanja wa Karume wakifuatilia burudani.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...