Naibu
Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe.Omary Mgumba, Amefanya Kikao na
watumishi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Mapema leo Jijini Dar es
Salaam akiwa safarini kikazi kuelekea Mkoani Ruvuma.
Naibu Waziri Mgumba amewasitiza watumishi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kufanya
kazi kwa bidii, ushirikiano na ueledi ili kutimiza dhima ya Serikali ya
awamu ya Tano ili kuleta maendeleo katika uzalishaji wa chakula kupitia
kilimo cha Uhakika cha Umwagiliaji kuelekea Tanzania ya viwanda.
Picha ya Pamoja Naibu Waziri Wizara ya Kilimo Mhe. Omary Mgumba akiwa na
baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Tume ya Taifa ya Umwagiaji katika Ofisi
za Wizara ya Kilimo Jijini dar es Salaam.
Katika Picha Naibu Waziri Wizara ya Kilimo Mhe. Omary Mgumba
akiongea na watumishi wa Tume ya Taifa ya umwagiliaji (hawapo pichani)
katika Ofisi za Wizara hiyo Jijiini Dar es Salaam, kushoto ni Bi Aida
Tesha Afisa Utawala Mkuu wa Tume hiyo.
Katika Picha ni baadhi ya watumishi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji
wakiwa katika kikao na Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Omary Mgumba.
Baadhi ya watumishi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji wakimsikiliza Naibu Waziri wa Kilimo Mhe . Omary Mgumba.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...