Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii

TAASISI ya moyo ya Jakaya Kikwete imefanikisha kufanya upasuaji kwa zaidi ya watoto 1000 ikiwa ni upasuaji mkubwa kwa watoto 600 na upasuaji mdogo kwa zaidi ya watoto 400. Akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mbio za Heart Marathon kwa mwaka 2019 Rais wa Tanzania Health Summit (THL) Dkt. Omary Chillo amesema kuwa mbio hizo zitafika kilele Aprili 28, 2019 katika viwanja vya Coco Beach ikiwa ni mara ya nne tangu kuanzishwa kwake na kusema kuwa malengo ya kuendesha mbio hizo ni kusaidia juhudi za serikali za kupunguza magonjwa yasio ya kuambukiza kwa kupitia michezo na kuchangia fedha kwa ajili ya watoto wanaohitaji upasuaji katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)

Aidha amesema kuwa zawadi zitakazotolewa ni pamoja na fedha taslimu zenye jumla ya thamani ya zaidi ya shilingi milioni 16 kwa wakimbiaji watakaokimbia mbio za kilomita 21, kilomita 5 na mita 700 kwa watoto na ameziomba taasisi mbalimbali nchini kuchangia na kushiriki katika mbio hizo kupitia tovuti yao ya www.heartmarathon.com ili kuweza kuokoa maisha ya watoto na wananchi kutoka katika janga la magonjwa yasiyoambukizwa.

Kwa upande wake Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto kutoka Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete Dkt. Naiz Majani amesema kuwa wanaungana na taasisi ya Tanzania Health Summit katika mbio hizo ili kuweza kuwachangia watoto wenye matatizo ya moyo kuweza kupata matibabu.

Dkt. Majani amesema kuwa kuanzia mwaka 2015 matibabu ya moyo yalianza kufanyika hapa nchini na hasa katika masuala ya upasuaji na hadi kufikia sasa jumla ya watoto 1040 wamepata matibabu ambapo watoto 600wamefanyiwa upasuaji mkubwa na zaidi ya watoto 400 wamefanyiwa upasuaji mdogo.

Pia amesema kuwa serikali imejipanga katika kuhakikisha matibabu yanatolewa nchini na hadi sasa wameshapatiwa wodi maalumu kwa ajili ya matibabu ya watoto pekee.Pia mmoja wadhamini hao kutoka Nexlaw Advocate, Wakili Upendo Mmbaga amesema kuwa ni mara ya pili wanadhamini mbio hizo ikiwa ni moja ya majukumu yao ya kusaidia huduma za afya hasa kuhusiana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza.

Aidha amewapongeza THS kwa kutoa hamasa kwa jamii na amezishauri taasisi na mashirika mbalimbali kushiriki katika kuelimisha umma kuhusiana na magonjwa hayo na wao kama Nexlaw Advocate wametoa jumla ya shilingi milioni 7 ili kuweza kufanikisha mbio hizo.


Rais wa Taasisi ya Tanzania Health Summit (THS) Dkt. Omary Chillo akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na msimu wa mbio za Heart Marathon kwa mwaka 2019 na kueleza kuwa tangu kuanza kwake 2016 zaidi ya watu 3000 wamekimbia na watu 1000 wamefanyiwa vipimo vya magonjwa yasiyoambukizwa, leo jijini Dar es Salaam.



Daktari Bingwa wa magonjwa ya Moyo kwa watoto kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Dkt. Naiz Majani akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mbio za Heart Marathon na namna taasisi hiyo ilivyofanikiwa na kufanya upasuaji kwa watoto zaidi 1000, leo jijini Dar es salaam


Upendo Mmbaga (kulia) akimkabidhi hundi ya shilingi milioni 7 Rais wa taasisi ya Tanzania Health Summit (THS) Dkt. Omary Chillo na kuhaidi kuendelea kushirikiana nao ili kufanikisha azma ya uelewa wa magonjwa yasiyo ya kuambukizwa kwa jamii na kuongeza nguvu katika juhudi za serikali za kukabiliana na magonjwa hayo, leo jijini Dar es salaam.(Picha na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii)


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...