Mlezi wa Serengeti Boys, Dkt Reginald Mengi amekutana na kikosi cha Srengeti Boys kilichotwaa ubingwa wa kombe la Cosafa, hivi karibuni nchini Botsw ana ili kuwapongeza.
Hafla hiyo ya chakula cha mchana ilihudhuriwa na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe, Rais wa TFF Wallace Karia na wadau wengine wa Soka.
Katika hafla hiyo Dkt Mengi aliwapongeza kwa ubingwa huo huku akiitoa zawadi ya fedha kwa wachezaji na benchi zima la ufundi huku akiwaambia kuwa kutwaa kombe hilo ni moja ya safari nzuri ya kuelekea kutwaa ubingwa katika michuano ya Afcon inayotarajiwa kurindima mwakani hapa nchini.Mengi amesema hii ni historia kwa nchi na pia timu hii ya vijana kufanya vizuri kwenye Mashindano makubwa mawili ikiwemo kombe la Cosafa na kurejea na Kombe, hivyo wanastahili pongezi.
“Pia niipongeze serikali kwa sapoti kubwa wanayoendelea kuitoa katika timu yangu hii ya vijana, hivyo tutampatia kombe hili mheshimiwa Rais Magufuli kama zawadi ya krismasi, kwani tunajua atafurahia kwakuwa ni mmoja ya viongozi wapenda mafanikio", alisema Mengi.
Amewaeleza kuwa, ana zawadi kubwa zaidi kwa vijana hao, ila amewasihi kuwa kuwaambia vijana hao wa Serengeti Boys kuwa zawadi hii ya leo ameipunguza baada ya kushauriwa kuwa umri wao ni mdogo sana hivyo kwahoyo yeye kama Mlezi na ataendelea kuwa nao atatatumia mali zake zote ili ahakikishe huko badaye maisha yao yanakuwa mazuri.
Kwa upande wa Waziri Mwakyembe amesema Kombe hilo ni zawadi ya sikukuu ya Krisimas kwa Rais Dkt John Pombe Magufuli na ameahidi atazifikisha salam zao kwake pamoja kuahidi kwenda kumkabidhi kombe hilo.

Mlezi wa Timu ya Vijana Serengeti Boys Dkt Reginald Mengi akizungumza na wachezaji wa Serengeti Boys na wadau wengine wakati wa hafla ya kuwapongeza Vijana hao iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe akitoa pongezi kwa timu ya vijana ya Serengeti Boys iliyofanikiwa kurudi na Kombe kwenye mashindano ya nchi za ukanda wa kusini COSAFA, hafla hiyo imefanyika leo Jijini Dar es Salaam.


Mlezi wa Timu ya Vijana Serengeti Boys Dkt Reginald Mengi akipokea kombe kutoka kwa Nahodha wa Serengeti Boys Abraham Morice na wakati wa hafla ya kuwapongeza Vijana hao iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...